ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, May 31, 2026

TANAPA YATINGA BRUSSELS KUELEKEA TUZO ZA KIMATAIFA ZA UBORA



Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ubelgiji, Mhe. Jestas Abuok Nyamanga, amwekaribisha ujumbe kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Nkoba Mabula, pamoja na maafisa kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), walipotembelea ubalozi huo mara baada ya kuwasili nchini Ubelgiji.

Ujumbe huo upo nchini Ubelgiji kwa ajili ya kushiriki hafla ya utoaji wa “Tuzo ya Kimataifa ya Mafanikio katika utoaji huduma kwa  Ubora kwa mwaka 2026” (Quality Achievement Award 2026), inayotolewa na taasisi ya kimataifa ya European Society for Quality Research (ESQR) 

Hafla hiyo inatarajiwa kufanyika tarehe 31 Mei 2026 katika Hoteli ya Le Plaza, Brussels.

Aidha, Mhe.Balozi Nyamanga amesisitiza kuwa uwepo wa ujumbe huo nchini Ubelgiji ni fursa muhimu ya kuendelea kuitangaza Tanzania, vivutio vyake vya utalii pamoja na kuonesha juhudi za TANAPA katika utoaji wa huduma bora kwenye jukwaa la kimataifa.






#ESQR2026 #QualityAchievementsAward2026 #TANAPA #MNRT #DestinationTanzania #Brussels #TANAPAGOApp

No comments: