Na Haruni Sanchawa, Bagamoyo
LILE Sakata la mtu aliyeuawa na wananchi baada ya kudaiwa kuwa ni mchawi aliyedondoka na ungo limefumuka upya baada ya gazeti hili kumpata mke wa marehemu aliyeamua kuweka mambo hadharani ambapo Uwazi limegudua kuwa, kumbe marehemu hakuwa mchawi, aya kwa aya zinazofuata zifafanua kila kitu.
Mke wa marehemu Ngosha, Bi.Fatuma Amini, akiwa na watoto wake, Tatu Kusekwa (kulia) na Kusekwa Kusekwa nyumbani kwao kijijini Makole wakati wakiongea na mwandishi wetu..
Tukio hilo lilitokea Mei, 16, 2010 maeneo ya Mbezi Shamba, jijini Dar es Salaam na kuacha gumzo kubwa nchini Tanzania. Marehemu alikuwa akiitwa Kusekwa Marando, al maarufu kwa jina la Ngosha,(41).
Mwandishi wa Uwazi, alifunga safari mpaka kijiji cha Makole, wilayani Bagamoyo, mkoani Pwani ambapo habari za awali za utafiti zilidai kuwa, marehemu alikuwa mkazi wa kijiji hicho na aliacha familia yenye mke na watoto wawili.

Familia iliyoachwa duniani na Ngosha. Kulia (mbele na nyuma) ni Ma Binti zake wa kufikia. Kushoto (mbele) ni Mama Mkwe wake,(mama mzazi wa mkewe) akiwa sambamba na wajuu na binti yake.
Uwazi lilibahatika kumpata mke huyo akiwa kwenye maoembolezo ya kifo cha mumewe huku mazishi yake yakiwa yamefanyika siku mbili kabla ya Uwazi halijafika kijijini hapo.
Awali, Uwazi liliongea na baadhi ya wakazi wa kijiji hicho ambao walikanusha kwa kusema kuwa, mpaka kuuawa kwake na wanachi wenye hasira, Ngosha hakuwa mchawi.
Habari zaidi zinadai kuwa, Ngosha alipelekwa Mbezi na mganga mmoja wa kienyeji (Uwazi linamchunguza) baada ya kumshawishi kwa pesa kuwa, atajifanya ameanguka na ungo akiwa safarini nje ya nchi ili yeye atakapotokea, amzindue kutoka katika hali ya uchawi na hivyo kuonekana ni mganga aneyeweza kazi.
Watu hao walizidi kusema kuwa, mganga huyo alimchukua Ngosha kutoka kijiji hicho na kwenda naye Dar huku marehemu akiiaga familia yake kwa ahadi ya kurejea baada ya siku mbili akiwa amekamilisha kazi hiyo na kumaliziwa kulipwa ujira wake.

wakiwa mbele ya nyumba yao
Habari zikafichuka zaidi na kudai kuwa, wanakijiji wawili waliotajwa kwa majina ya Aweso Kabanga na Ramadhan maarufu kama Bonge ndiyo waliofika kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Makole, Mei 13, 2010 wakadai walikuwa wakitafuta mtu wa kwenda naye Dar kufanya kazi maalum kwa muda wa siku mbili.
Uchuro zaidi wa habari unasema kuwa, wakati watu hao wanatoa ombi hilo kwa Mwenyekiti alikuwepo kijana mmoja aliyetajwa kwa jina la Msafiri Suleiman na wakamuomba wamchukue yeye kwa mapatano ya kulipwa shilingi 200,000 lakini kabla ya kuondoka angetanguliziwa shilingi 50,000 .

Mwandishi wetu alifika ofisi ya serikali ya Kijiji na kuongea na Mwenyekiti wake juu ya suala hili. Hii ndiyo ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Makole, Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Makole, Bw. Anthony Muhode (kulia) akiwa na Katibu wake Mtendaji, Bw. Kibuna Said
Maskini, kumbe sikio la kufa huwa halisikii dawa, Msafiri alikataa na kusema Ngosha ndiye mwanaume pekee ambaye angeiweza kazi hiyo ngumu.
Ndipo walipomtuma Msafiri huyo huyo awaitie Ngosha ambaye alipofika alikubali kwa kupokea kwanza shilingi elfu hamsini, kumbe alikuwa akikabiliana na kifo cha aibu.
Ilikuijua kwa undani zaidi habari hii ya kutoa machozi, Uwazi liliongea na mke wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Fatuma Amini (33) ambaye alikiri kuwa, ni kweli kuna mtu anaitwa Aweso na mwenzake Ramadhan walifika kwake na kumwomba mumewe wasafiri naye Dar wakidai kuna kazi ya kufanya kwa muda wa siku mbili.

..hapa ndilo kaburi la Ngosha kama anavyoonesha mke wa marehemu
Huku akibubujikwa machozi kila wakati kwa kumkumbuka mumewe aliyemwachia ulezi wa watoto, Bi. Fatuma alisema:
“Msafari ndiye aliyekuja nyumbani kumwita mume wangu kwenda kwa Mwenyekiti wa Kitongoji, alipofika aliwakuta watu hao kutoka Dar wakiwa wanakunywa pombe ya kienyeji huku wakiendelea mazungumzo.

..watoto wa marehemu Tatu na Kasekwa wakiwa makaburini
“Muda mfupi watu hao na mume wangu walikuja hapa nyumbani kuniaga, mume wangu alisema
anaondoka kwenda Dar kwa ajili ya kuwafanyia kazi fulani watu hao,” alisema mwanamke huyo na kuanza kulia.
Aliponyamza, aliendelea: “Licha ya kwamba waliniaga, lakini wale watu hawakufafanua aina ya kazi ambayo mume wangu anakwenda kuifanya, lakini kwa uzoefu, mume wangu alikuwa ni mtu ambaye anatunza familia kwa kufanya vibarua mbalimbali, hivyo niliamini hata Dar anafuata hicho, kumbe masikini anafuata kifo chake,” alisema Bi. Fatuma huku machozi yakimshuka mashavuni.
Akionekana anajitahidi kujikaza kwa kifo cha mumewe kipenzi, mke huyo alisema kuwa, alianza kupata wasiwasi baada ya kuona zimepita siku tano mumewe hajarudi nyumbani na watoto walikuwa wakimulizia wakisema mama, baba yuko wapi!
Anasema: “Ilibidi niende kwa Msafiri ambaye alikuja nyumbani kumchukua mume wangu, yeye akaniambia kuwa, hakuondoka naye, labda ajaribu kuulizia kwa Ramadhan ambaye ndiye aliyekwenda naye Dar es Salaam.”
“Sasa ikawa sijui lolote, mume wangu haonekani, hakuna kinashosemwa, yaani hali niliyokuwa nayo, mungu mwenyewe anajua,” alisema Bi. Fatuma na kushindwa kuendelea kwa kilio.
Habari zaidi zinasema kuwa, marehemu alipofika Dar kwa mganga huyo wa kienyeji (jina tunalo) ambaye ni mkazi wa Kimara aliambiwa upya kazi aliyotakiwa kuifanya na mapatano mapya ya pesa ambapo angemaliziwa kulipwa shilingi 150,000 baada na kutanguliziwa shilingi elfu 50 kule kijijini. Mke wa marehemu alisema pesa alizoachiwa na muwe, ni shilingi elfu kumi tu.
Uchunguzi huo uliofanywa na gazeti hili kwa muda wa wiki tatu sasa kuhusiana na sakata hilo ulibaini kuwa, siku ya tukio sasa, marehemu Ngosha alipakwa masizi mwili mzima na kutengenezewa dawa kadhaa za kienyeji kisha kuwekwa kwenye ungo ili aonekane alikuwa anaruka na ungo huo na akadondoka kisha akafundishwa kwamba, akiulizwa na raia aseme alikuwa akisafiri kwenda Shelisheli kwenye mkutano wa wachawi.
Habari zinasema kwamba, marehemu bila kujua roho ya mauti i mbele yake, alikubali mpango huo na muda ulipofika, alitolewa nje ya nyumba ya mganga huyo na kuwekwa barabarani ili watu wamwone kwa lengo kuwa, baadaye mganga angejitokeza na kumuagua kisha ajifanye amepona, shabaha ikiwa kumpa umaarufu sangoma huyo kwa watu watakaoona tukio hilo.

Marehemu Ngosha alikuwa mkulima, amecha shamba la mahindi la ekari tatu kama mkewe alivyomuonesha mwandishi wetu
Hata hivyo, baada ya kufanywa hayo, wananchi walipomwona Ngosha hawakusikiliza madai yake kwamba, alikuwa safarini Shelisheli na hata pale mganga huyo alipotokea, naye walimpuuza na kuanza kumpiga kwa zana mbalimbali licha ya kuomba asiuawe akisema ametoka Shinyanga.
Imedaiwa kuwa, mganga huyo alimkimbizia ndani Ngosha ili kumwokoa lakini maelezo yake yalizidisha hasira kwa watu ambapo walivunja mlango wa nyumba ya sangoma na kumtoa nje ‘mchawi’ huyo na kuendelea kumpiga mawe hadi kifo chake.
Habari zinasema wananchi waliamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuhamasishana kuwa, wachawi kama Ngosha ndiyo wanaokwenda eneo hilo kuchukua watu na kuwafanya misukule.
Uchunguzi umebaini kuwa, kilichomponza Ngosha ni kukubali kusema kama alivyoagizwa na mganga huyo ambaye licha ya kuishi Kimara inasemekana ana mji mwingine huko maeneo ya Tanita, Kibaha.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema baada ya Ngosha kuuawa, polisi walishindwa kutambua ndugu zake na mwili ukachukuliwa kupelekwa Hospitali ya Tumbi, Kibaha ulipohifadhiwa kwa siku 23.
Habari zinasema ilikuwa imebakia siku moja ili Ngosha azikwe na Manispaa ndipo ndugu zake walipohangaika na kufanikiwa kwenda kuitambua maiti na wakaichukua. Alizikwa Juni 8, 2010 huko kijijini kwake Makole, Bagamoyo.
Hata hivyo, baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wetu wamewashauri raia kuacha kujichukulia sheria mkononi kwani Ngosha angepelekwa polisi mganga anayedaiwa kufanya utapeli huo angekamatwa na kushughulikiwa na dola lakini badala yake kituoni kumebaki ungo na tunguli tu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Elias Kalinga alisema upelelezi wa tukio hilo unafanyika
No comments:
Post a Comment