MTOTO WA AFRIKA KUNDUCHI BEACH
Hayo yalisema leo jijni Dar es Salaama na Mfanyabiashara Salehe Bin Zoo alipokuwa akisherekea na watoto hao wa mitaani katika Hoteli ya Kunduchi Beach .
Salehe Bin Zoo alisema kuwa tatizo la watoto wa mitaani ni la kila mmoja hivyo ni jukumu letu kujitokeza na kuwachangia pasipo kuchoka.
“Kila mmoja anapaswa kuwachangia watoto hawa wa mitaani ikiwemo huduma ya maradhi, chakula na huduma ya Afya” alisema Bin Zoo.
Kwa upande wake Omari Rajabu ambaye anawaongoza watoto hao wa mitaani walio jijini Dar es Salaam ‘ Maalufu kama New Hope Family Street Children” aliomba jamii ijue bna itambue kuwa watoto wa mitaani ni lulu kwa Taifa la leo na lijalo.
Ambapo alisema kuwa wengi wa watoto hao wa mitaani wamejikuta wakikimbilia mijini kwa matatizio mbalimbali na kujikuta wapo mitaani, pia wengi wanakimbia mateso katika familia ikiwemo kunyanyaswa na mama wa kambo ama familia duni.
Hivyo kwa umuhimu wa mtoto wa Afrika ni jukumu lao kushirikiana kwa pamoja na watoto wote wa Afrika, ilikusherekea kwa pamoja.
Watoto hao walisema kuwa wanakumbana na majanga mbalimbali mitaani ikiwemo ya kunyanyaswa ilihali tu wao ni watoto wa mitaani na kukosa fursa kwa jamii.
watoto hao walisema kuwa mpaka sasa wanaendelea kutafuta wadhamini na wafadhiri ili wawasaidie katika kupigana vita ya kuwakomboa watoto.
'Siku ya leo ya mtoto wa Afrika ni siku pekee ya kuwakumbuka watoto wa mitaani iliwaweze kujiona wanafarijiwa na jamii iliyowazunguka" alisema Omary Rajabu.
Mpaka sasa kikundi hichi kinaishi nje na akina ofisi maalum kwani kila mambo ya kiofisi yanafanywa mitaaani, ambapo maali kuu ni pale bostani ya Posta.
Kwa upande wake mgeni mwalikwa wa sherehe hizo, Nimka Lameck (10), ambaye ni Mwenyekiti wa Chipukizi Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Mkutano Mkuu Taifa Chipuki na Mwanaharakati wa Haki za binadamu ameitaka Serikali kutunga sheria kali kwa wanaonyanyasa watoto.
“Watoto wa leo ndiyo muongozo wa Taifa lijalo hivyo hatunabudi kujengewa misingi thabiti nay a dhati k wa jamii iliyotuzunguka hususani watoto wa mitaani ambao ni nuru ya maisha ya sasa na baadae” alisema Nimka.
Aidha, Kaka Mkuu wa watoto hao Kizo Said ambaye anawasaidia kila jambo watoto wa mitaani ambao wengi wanakabiliwa na matatizo,
Alisema kuwa, watoto hao mara zote wanalala nje bila msaada wowote pamoja na hilo Serikali bado haijaweza kuwatilia kipaumbele na mkwazo wa kuwaongoza vyema.
“Kampeni za malaria zinaamasishwa lakini sisi watoto wa mitaani hatukumbukwi, hali hii inatupelekea na kuona kama tumetengwa na viongozi wetu’
Pia waliomba jamii ijitokeze kwa kusaidia watoto wa mitaani na kuwakomboa kwa namna moja ama nyingine.
Kwa upande wake, Chacha Muta (15), ambaye aliongea kwa niaba ya watoto hao wa mitaani alisema kuwa matatizo wanayokabiliana nayo Serikali inayapuuzia kwani wanatendewa mambo mengi bila msaada wowote.
“Tunaiomba Seriakali kutupia jicho sisi wa mitaani, kwani mara zote tunakula vyakula vya majalalani,tunalala nje nab ado tunaitwa vibaka jamani sisi ni kama watoto wengine’ ..Chacha alisema kwa machungu huku akibubujikwa na machozi.
Siku ya mtoto wa Afrika inasherekewa Afrika nzima kila Juni 16 ambapo mwaka huu inafanyika kila mkoa ambapo umoja wa watoto hao waliweza kusaidiwa msaada wa kusherekea siku hiyo katika hoteli hiyo ya Kunduchi.
No comments:
Post a Comment