ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 25, 2010

Malkia wa Bendi ya FM Academia

Malkia wa Bendi ya muziki wa dansi nchini, FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, Ketula Kihongosi ‘Kei’, ameibuka na kuweka wazi sababu zilizomfaya kupigwa picha za utupu ambazo zilisambazwa kitaani.

Akipiga stori na Ijumaa, hivi karibuni alipokuwa viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es Salaam, Kei alisema kuwa, mvuto wa umbo lake ndiyo sababu kubwa ya yeye kupigwa picha hizo kwani aliyemfotoa alichanganywa nao hivyo ilikuwa ni lazima tukio hilo litokee.

“Mimi naamini aliyenipiga picha zile chafu alichanganywa na mvuto wa umbo langu, kwani muda mrefu alikuwa akisema anapenda kuwa na picha zangu kwenye simu yake ili awe ananiangalia hata akiwa hayupo na mimi,” alisema malikia huyo.

Pamoja na kuweka wazi sababu hiyo ambayo yeye anaiamini, mrembo huyo aliendelea kuomba radhi kwa watanzania wote, ndugu jamaa na marafiki na kuwataka wasimuelewe vibaya zaidi ya kuona jambo hilo mwenyewe hakulikusudia.

Mwisho alimalizia kwa kusema kuwa, ana imani kwamba, aliyemfanyia uovu huo anamhusudu sana hasa umbo lake, akijua ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto kati ya wanawake aliowahi kutembea nao.

“Naamini mimi ndiye mwanamke pekee mwenye mvuto kati ya wanawake aliyowahi kutembea nao na ndiyo maana amediriki kunipiga picha, mbona wengine hajawafanyia hivyo?” Alihoji kwa kujiamini Ketula

No comments: