Ajinyonga kwa ugumu wa maisha
na Andrew Chale
MCHINJA nyama machinjio ya Vingunguti Chidole Chilimaus Gonda (28) amejinyonga na kuacha ujumbe juu ya uamuzi wake huo
Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa tano asubuhi huko maeneo ya Vingunguti Becco,.ambapo inadaiwa marehemu ambaye ni mkazi wa eneo hilo.
Ambapo inadaiwa alikutwa ndani ya chumba akiwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani aliyoitundika kwenye kenchi ya nyumba.
Kamanda Shilogile alisema kuwa marehemu aliacha ujumbe wa maandishi uliosema; “Nimeamua kujinyonga kutokana na ugumu wa maisha”. Maiti ya marehemu huyo imehifadhiwa katika Hospitali ya Amana na upelelezi unaendelea.
Katika tukio jingine garia aina ya Nissan Terrano lililokuwa na namba za usajili T 918 AAA, la Mchumi wa Wizara ya Afya, raia wa Ujerumani, Meinolf Kupper (52) liliwaka moto na kuteketeza vitu vyote.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Eliasi Kalinga alisema tukio lilitokea jana majira ya saa saba na nusu usiku ambapo liliwaka moto ghafla na kuteketeza vitu vyote vilivyokuwemo humo.
Kalinga alisema gari hilo lilikuwa limeegeshwa nje ya nyumba yake, ambapo chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme wa betri ya gari hilo.Thamani nzima ya katika tukio hilo bado hajajulikana na moto ulimwa na kikosi cha Ultimate Security na uchunguzi unaendelea
No comments:
Post a Comment