MT.ZION
BONGO DC
Kidumbwe dumbwe ya ile mechi iliyoleta kizazaa mpaka kutishia kuanzishwa timu nyingine inayojiita BONGO REAL FC sasa kurudiwa jumapili June 27 pale pale wanja jipya la Kalmia.
Hii itakuwa burudani tosha kwa wakazi wa DMV,mechi iliyopita ilikua ngumu na BONGO DC ilionekana kushinda mechi hii kutokana na kupiga mipira mingi golini zidi ya MT.ZION lakini bahati haikua yao na kizingiti kikubwa alikua golikipa mahili wa MT.ZION aitwae Willy ambae ameishacheza ligi kuu kwao Cameroun
Mechi hii imeshakua gumzo kubwa mjini,hasa kutokana na mmiliki wa timu ya MT.ZION anapopata ugonjwa wa moyo timu inafungwa,kwa hiyo anahakikisha anakusanya wachezaji kila pembe ya Dunia ili apate ushindi.
Kwa upande wa BONGO DC wao wanasema wanajaribu bahati yao tena kwani mechi iliyopita iklikua ngumu sana kwao kwani jamaa ni wazuri sana na ni timu iliyo fit kila idara kwa hiyo tutajitahidi kutoa burudani kwa mashabiki wa soka.
Tunajua mechi ni ngumu sana lakini tunapeleka timu kwa ushindani,sio Bora liende,kwa hiyo tunawaomba mashabiki wafike kwa wingi mechi hii itakua burudani tosha wikiendi hii
No comments:
Post a Comment