ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 16, 2010

Mwanamitindo akipigwa picha za uchi amuudhi mkulima

Mkulima Wen akiwafukuza wanafunzi waliokuwa wakimpiga picha mwanamitindo ambaye amekaa uchi pembeni.
MKULIMA Hu Wen wa Zhengzhou mashariki mwa China, alilishambulia kundi la wanafunzi wa somo la sanaa baada ya kuwakuta wakimpiga picha mwanamke mmoja aliyekuwa uchi katika shamba lake ambapo aliwashambulia kwa kuwachapa bakora wakakimbia.

“Wanafunzi hao na watalii walikuwa wanampiga mpicha msichana huyo,” alisema Wen akiongeza kwamba hajutii kuwashambulia watu hao ambao waliripoti polisi tukio hilo.

“Sitaki watu waovu kama hao ambao huchora picha za matusi kwenye miamba ya shambani mwangu na kupiga picha za uchi,” alisema mkulima huyo ambaye hakumshambulia msichana huyo bali alimsaidia kuvaa nguo zake na kumwonya kuacha tabia hiyo mbaya. 

No comments: