ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 10, 2010

PAUL AITABIRIA HISPANIA USHINDI PAMOJA NA UJERUMANI

Pweza akiingia katika kisanduku chenye bendera ya Hispania kuashiria kuwa nchi hiyo ndiyo wataibuka mabingwa wa michuano hii ya kombe la dunia
Pweza Paul amezitabiria ushindi timu za Hispania pamoja na Ujerumani katika utabiri alioufanya leo. Pweza huyo ambaye ametabiri sawa mechi zote za timu ya Ujerumani katika fainali zinazoendelea za kombe la dunia, leo ametabiri kwa mara ya kwanza mechi ambazo timu ya Ujerumani haihusiki pale alipotabiri kuwa Hispania ataishinda Uholanzi katika fainali itakayofanyika siku ya jumapili julai 11, 2010. Vilevile Paul ameitabiria vizuri timu yake ya Ujerumani kuwa itaifunga Uruguay katika mechi ya kumtafuta mshindi wa tatu wa michuano hiyo hapo kesho
Pweza Paul akiitabiria UJerumani ushindi dhidi ya Uingereza
Kati ya mechi 12 amepatia mechi 10 sawa na asilimia 83 na kukosea mechi mbili tu!
CHANZO GLOBAL PUBLISHERS

No comments: