ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 22, 2010

Ziara ya Vodacom Miss Tanzania KINAPA

Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiwa wamebeba mabegi mgongoni mithili ya watalii wanaoteremka mlima Kilimanjarto wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakiangalia michoro ya ramani ya Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kialimanjaro (KINAPA) wakati warembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini.
Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), David Loosurutia (kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya mazingira ya hifadhi hiyo kwa warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakati wa rembo hao walipotembelea KINAPA jana. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini
Baadhi ya warembo wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakizungumza na mmoja wa vijana wanaojishughulisha na kazi ya kusindikiza watalii kupanda Mlima Kilimanjaro jana wakati warembo hao walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) iliyopo Marangu mkoani humo. Warembo 30 wa Vodacom Miss Tanzania wapo katika ziara ya kuhamasisha utalii wa ndani katika mikoa ya Kanda ya Kaskazini. 
(Picha na Mpigapicha wetu kwa hisani ya Global Publishers).

No comments: