Balozi Sefue akijibu risala iliyosomwa na Mama Munanka kwa niaba ya wafanyakazi wa Ubalozi Washington,DC,risala iliyotoa shukurani kwa kazi nzuri aliyofanya ikiwemo juhudi alizofanya mpaka kupatikana kwa jengo jipya la Ubalozi na kwamba kwa kufanya kazi kwa kujituma kumewezesha Marekani kuwa nchi inayoongoza kwa kupeleka watalii wengi Tanzania.
Mama Munanka pia alimzawadia Mh.Sefue zawadi kwa niaba ya wafanyakazi wote.
Mh.Sefue akijibu risala,alianza kwa kuwashukuru wafanyakazi wote kwa ushirikiano waliompa kwa kipindi chote cha miaka mitatu na kuomba ushirikiano huu wampe Balozi Maajar.
Mh.Sefue aliendeleaa kusema,kitu ambacho hakukipendelea ni kuona Jumuia ya Watanzania wanaoishi Washington Metro Area ikisambaratika,na kusisitiza ni lazima utafutwe ufumbuzi haraka iwezekanavyo kurudisha uhai wa jumuiya.
Anasikitishwa sana na hali na ameshauri na kuwaomba Wanajumuia wakae chini wamalize tofauti zao,kwani hapa Washington ndio makao makuu ya Serikali ya Marekani pamoja na zilipo ofisi za Ubalozi wa Tanzania pamoja na makazi yake.
Alieleza kwamba Watanzania waishio hapa DC hawana budi kuiga mfano wa Jumuiya nyinginezo za Watanzania waishio katika mikoa mbali mbali ya Marekani kama vile Ohio,Minnesota na California ambao wana uongozi na Jumuiya zenye upendo na kuheshimiana.
No comments:
Post a Comment