Wednesday, August 25, 2010

FOLENI NDEFU YA MAGARI DUNIANI

Foleni ambayo imevunja rekodi duniani kwa urefu.
• IMECHUKUA SIKU KUMI SASA KATIKA JIJI LA CHINA
FOLENI iliyovunja rekodi duniani imetokea katika barabara kuu ya kutoka Beijing kwenda Zhangjiakou huko Huailai, katika jimbo la kaskazini mwa China la Hebei ambapo imeenea katika urefu wa kilomita 96.

Kitu cha ajabu ni kwamba alama zote za barabarani za kuzuia msongamano wa magari, zinafanya kazi ili kuzuia foleni inayosababishwa na maelfu ya malori yanayosomba mkaa na kuuleta katika jiji hilo.

Hata hivyo, foleni hiyo imeleta baraka kwa “wamachinga” wanaouza bidhaa zao kwa wingi kando ya barabara hiyo, ambapo huuza sana mayai, maji na sigara kwa madreva ambao wanaonekana kukata tama.

Zaidi ya hapo, wezi wamekuwa wakichomoa bidhaa mbalimbali kutoka katika foleni hizo wakati madreva wakiwa wamelala. Vitu hivyo ni pamoja na petroli.


NA GLOBAL PUBLISHERS

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake