
Mlinzi huyo akiwa amefungwa kamba na mbele yake kuwekewa chupa tupu za bia ya Serengeti
Na Dunstan Shekidele, MorogoroULE usemi unaosema kwamba mlinzi hatakiwi kupewa godoro, ulijidhihirisha kwa kijana huyu ambaye ni mlinzi katika hoteli ya Dolphin iliyopo nje ya uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro ambapo mwajiri wake aliamua kumpa kiti cha kupumzikia wakati akilinda usalama katika hotel hiyo.
lnadaiwai kwamba baada ya mlinzi huyo wa mchana kukaa kwa muda mrefu kwenye kiti hicho, alijikuta akipitiwa na usingizi mzito ambapo baadhi ya wafanyakazi wenzake walimdhihaki kwa kumfunga kamba na kumwekea lundo la chupa tupu za bia.
Wafanyakazi hao walidai kwamba mlinzi huyo alifika katika lindo hilo akiwa “amepambwa”: na harufu ya pombe, kitu kilichomsababishia uchovu na kushindwa kufanya kazi hiyo ya ulinzi
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS
No comments:
Post a Comment