ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 16, 2010

MPATIE KAZI YA ULINZI SEMBULI!

NA DUNSTAN SHEKIDELE,MOROGORO
AMINI USIAMI jamaa mmoja ambaye ni mlemavu wa miguu [Kiwete] ameamua kutafuta kazi ya ulinzi, huku akidai kwamba licha ya ulemavu alionao kazi ya kuombaomba anaichukia mno na ndiyo maana ameamua kufanyankazi hiyo bila kupitia mgambo.

Mwandishi wetu alimkuta Mlemavu huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Sembuli Muhidini, mkazi wa Chamwino mkoani hapa, na kudai kuwa amevaa nguo hizo kwa lengo la kutafuta kazi ya ulinzi wa mchana.

Alipoulizwa kwamba nguo hizo amezipata wapi, alisema kwamba awali alikuwa akiuza mitumba kabla ya mtaji wake kukata hivyo katika moja ya marobota ya mitumba kutoka Ufilipino aliyofungua alizikuta nguo hizo pamoja na kofi yake. Sembuli anaomba kazi ya ulinzi, lakini iwe ya mchana tu ambayo anaamini ataiweza!

PICHA KWA HISANI YA GLOBAL PUBLISHERS

No comments: