Timu ya Houston(Serengeti Boyz)


Timu ya Wichita(Ngorongoro Heroes)

Stars United(Kandanda Safi Kiwango cha T.B.S.)
Na Mwandishi Wetu
Timu ya Houston (Serengeti Boyz) itaondoka Ijumaa usiku kuelekea Wichita kwa mpambano na timu ya huko unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Wichita.
Akiongea na VIJIMAMBO Alune Mwasa amesema timu itasafiri na wachezaji 18,kocha,kiongozi na Daktari.Timu itakodisha SUV 3 zenye uwezo kubeba watu saba saba.
aliendelea kusema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri kimchezo na wameahidi ushindi mnono,hawa jamaa walituotea last time kila siku sio jumapili.
Akiwajibu Houston,timu kepteni wa Wichita Diwani Cheche,amesema mpira hapa ndio chuo kikuu,wao ni shule ya vidudu sasa Mpwa wewe pima mwenyewe,nani zaidi????
Wakati huo huo Timu ya Stars United itaelekea Atlanta GA,Aug 14,kwenye mpambano na timu ya Wakenya,Jamhuri ya huko,wenyeji wamsema wanaisubrii kwa hamu kubwaStars na tupo tayari kwa mpambano.
Wachezaji watakao andamana na timu ni kutoka NY,Ebra Nyagaly,NJ Tif Maali,DC,Libe Mwang'ombe,Ra.sheed Beach Boy,Yahaya Kheri,Mchili,Adam NY,Gilles,NC ni Shabani Mwapambe,Feisal Omar,Simon Marko,Hamfrey Owen,Alisha Mundo ambao wataungana na wenzao wa Atlanta,GA,Hadji Helper,Liga Hamza,Juma Hadikubwa,Elvis Dotto,Abel na kuongezewa nguvu na Fred Mburushi na wengineo wabongo wa ATL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake