Refa Kenyatta(Manyoto Ndimbo)
Refa Ritch Richie

Kikosi Cha Mauji Yanga

Kikosi Cha Mnyama Mkali Simba
Ule mpambano unaosubiliwa na wakazi wa DMV na vitongoji vyake umeingia kwenye utata wa refa gani achezeshe mpambano wa Simba na Yanga,
Kwa upande wa Yanga hawamtaki Kenyata kwa sababu mechi ya mwisho ya mahasimu hao walimuaona amekaa benchi la ufundi Simba,na aliingia uwanjani kubishana na refa na wachezaji wa Yanga akitaka refa aipatie faulu Simba,mashabiki wa Yanga walisikika wakisema"kaka Kenyata ni Lunyasi damu yule atutaki achezeshe mtanange huu atapendelea kaka"

picha ya Kenyata iliyonaswa akibishana na wachezaji wa Yanga akisisitiza ipigwe faulu golini kwa Yanga.
Kwa upannde wa Simba wao hawamkatai Ritch Richie kuchezesha "ni refa mzuri lakini tunadhani ni Yanga"Licha na malumbano hayo ya refa,kambi zote ziko shwari na kila upande ukidai ushindi dhidi ya mwenzake.
kitu kingine ni kuhusu uwanja,inasemekana Simba haitaki kuchezea mechi Kalmia kwa sababu inadai haina bahati na uwanja huo,inataka mpambano huo uhamie Meadowbrook park.
Yanga wanasema kumfunga Simba ni kama kumsukuma mlevi,sisi kokote wanakotaka Simba sisi tutacheza nao tu.
Mechi hiyo itakua ni moja ya sherehe za Labor Day Weeekend zitakazo anza rasmi ijumaa ya Sept 3 kwenye ukumbi wa Mirage na kufuatiwa na mechi ya Kenya na Tanzania Itakayochezwa Jumamosi,Kalmia.

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake