ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 21, 2010

UZINDUZI KAMPENI CCM: JK ADONDOKA, AREJEA JUKWAANI

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi, ambaye pia nia Rais, Mh Jakaya kikwete amedondoka akiwa jukwaani wakati akielezea sera na mafanikio ya Chama Chake katika mkutano mkubwa wa ufunguzi wa kampeni uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es salaam dakika chake zilizopita! Mara baada ya kudondoka, uwanja mzima ulitaharuki, lakini viongozi wengine wa chama, wakiongozwa na Katibu Mkuu, Mzee Yusuf Makamba, waliwatuliza wanachama. Baada ya dakika zipatazo 10 au 15, Mh. Rais alirejea jukwaani na kuendelea na hotuba yake kwa muda mfupi kabla ya kumaliza na kuwaaga wanachama wake na kuondoka jukwaani. Tukio la leo, linakumbusha lile la mwaka 2005 ambako Rais alidondoka katika viwanja hivyo wakati akifunga kampeni za chama. Picha hii ilipigwa muda mfupi baada ya Mh. Rais kupanda jukwaani kwa mara ya pili kuhutubia
 
Rais Kikwete akihutubia wanachama mara baada ya kudondoka na kurejea tena jukwaani katika viwanja vya Jangwani Dar es salaam, Aug 21, 2010
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: