ANGALIA LIVE NEWS
Monday, August 16, 2010
Wagombea Ubunge Kinondoni,Ubungo na Kawe wachukua fomu
Na Andrew Chale
BAADHI ya wawania kiti cha Ubunge katika majimbo ya Kinondoni,Kawe na Ubungo wamechukua fomu rasmi ilikutambulika na tume ya uchaguzi katika kinyang’anyiro kinachotalajiwa kuanza Agosti 20.
Fomu hizo zilizokua zikitolewa katika ofisi za manispaa ya Kinondoni, ambapo wagombea wa vyama mbalimbali vya siasa waliweza kuchukua fomu hizo ambazo wanatalajiakuzirudisha Agosti 19 siku moja kabla ya kuanza kampeni.
Awakiwa wa kwanza kuchukua, mgombea wa Ubunge jimbo la Kinondoni kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),Phillip Nyanchin Mogendi ‘Phinyamo’ aliwaambia waandishi wa habari kuwa atahakikisha analinyakua jimbo hilo na kutekeleza mambo mbalimbali kwa kutumia uwezo wake alionao.
“Mimi kwa uwezo wa uongozi na elimu niliyopata, ni chachu kwa kuwainua wananchi wa jimbo hili la Kinondoni ambalo muda mwingi viongozi wamewageuza wananchi vichwa vya kinolea” alisema Phinyamo.
Mbali na mgombea huyo wagombea wengine ni Halima Mdee jimbo la Kawe kwa tiketi ya Chadema, ambapo alisema atatumia silaha za maangamizi tisa, ambayo atatoa ukweli kwa wananchi juu ya CCM kilivyo fanya ufisadi kwa kujilimbikizia mali na kuuza maeneo ya wazi.
Wengine jimbo la Kinondoni Idd Azzan (ccm) ambapo aliomba wananchi waendelee kumuunga mkono ilikufanikisha yote aliyoyaanza.majimbo mengine Hawa Ng’umbi (CCM) jimbo la Ubungo huku jimbo la Kawe alichukua Angela Kizigha.
Wagombea hao walifika kuchukua fomu hizo wakiwa na wapambe wao wakisindikizwa sambamba na madiwani wao.
Kwa mujibu wa msimamizi msaidi wa uchaguzi jimbo la Kinondoni, Levis Mnyambwa aliwataka wagombea hao kuzijaza fomu hizo vizuri na kuzirudisha Agosti 19 ilikuzihakiki na kutambuliwa rasmi kugombea ubunge kwa wananchi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment