Akina mama kutoka sehemu mbalimbli wakiwa Kariakoo jijini Dar es Salaam wakitafuta bidhaa madukani kwaajili ya kujiandaa na sikukuu ya Iddi.
LEO ni siku ya 21 tangu waumini wa dini ya Kiislamu walipofunga baadhi ya watu waliokutana na mpiga picha wetu wanalalamika kuwa bidhaa zimepanda bei hasa nguo za watoto, baadhi ya akina mama wamelalamikia hali hiyo.Wanafunzi wa shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko nao hawako nyuma katika kujipatia vifaa vya elimu ili kujiongezea maarifa, hapa wanaonekana wakichagua vitabu kama ambavyo wamekutwa na kamera yetu leo Kariakoo jijini Dar.
Biashara ya pikikipki imeshamiri ambapo sasa inasemekana zimeshuka bei na kufanya watu wengi kumudu kuzinunua kama alivyokiri muuzaji huyu aliyejitambulisha kwa jina la Hussein Ally, anasena bei ni karibu na bure.
Baadhi ya waumini wa dini ya kiislamu wakichagua kofia ambapo mmoja wa wanunuzi aliyejitambulisha kwa jina la Ustaadhi Juma alisema wananunua ikiwa ni maandalizi ya sikukuu ya Iddi.
Askari wa Jiji wakiwa wamemzingira kijana ambaye hakujulikana jina akiwa amebeba madumu aliyoyakusanya kutoka maduka mbalimbali, haikujulikana anayapeleka wapi.
Kijana mmoja ambaye hakutambulika jina na ofisi anayofanyia kazi akizoa takataka kutoka kwenye mkokoteni na kuzipakia katika tela bila kuwa na vifaa vya kujikinga mikononi (gloves) au buti pamoja na kifaa cha kuzuia vumbi puani. Hii ni hatari kwa afya yake.
PICHA ZOTE NA HARUNI SANCHAWA WA /GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake