Advertisements

Monday, September 20, 2010

Tangazo


NDUGU WATANZANIA,
Kama mlivyofuatilia kisa cha ndugu yetu (Amouri)ama kama ajulikanavyo kwa jina la Abraham Allen aliyefariki 9/9/2010 huko Harrisburg,PA.
Taarifa tulizozipata muda mfupi uliopita ni kwamba kutokana na uchache wa muda na ugumu wa ukusanyaji wa michango kutoka kwa wanafamilia kule Tanzania,uwezekano wa kusafirisha mwili wa marehemu ili akasitiriwe nyumbani umeshindikana na hivyo familia ya marehemu imeomba asitiriwe hapa hapa.Kwa mila na desturi zetu jumuiya za waTanzania zimeamua kukamilisha taratibu za mazishi ya marehemu Amouri katika taratibu za dini yake ya kiislam.Ili kufanikisha taratibu hizo kiasi cha Dola elfu tatu ($3000.00)kinahitajika haraka iwezekanavyo.
Jumuiya ya Watanzania ya New York na vitongoji vyake(New York Metropolitan Tanzanians Community) ikishirikiana na Jumuiya ya Waislamu ya washington(TAMCO)pamoja na Ubalozi wetu wa Washington unawaomba Watanzania popote walipo kuwasilisha michango yao ili tuweze kuusitiri mwili wa Marehemu.


TUMA MCHANGO WAKO KWA,
TANZANIA MUSLIM COMMUNITY,
CAPITAL ONE(CHAVE CHASE BANK)
ACC # 0944380077.

KWA WAKAZI WA NEW YORK WASILIANA NA,
HAJJI KHAMIS-347-623-8965
SHABANI MSEBA-347-712-8539.

KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA,
YACOB KINYEMI 202-629-7841
MGANGA 202-374-0988
SHABANI MSEBA 347-712-8539

ASANTENI.

No comments: