Bi Kidude Atinga Fleva Nite Ya Mzalendo Pub Usiku Wa Kuamkia Leo Nakutunzwa Mikwanja Kibao
"......aaaahhhhh.... ahmadaa eehhh,ahmadaaa........ Umelewaaa" Bi. Kidude akisakata magoma usiku wa kuamkia leo ndani ya kiota cha maraha cha mzalendo Pub Jijini Dar es salaam.
Dj Mackay akimkaribisha Bi. Kidude ndani ya flava nite huku akimuhesabia Bi. Kidude kitu cha jiwe (shilingi laki moja bila chenji) kama ishara ya baraka walizopokea kutokana na ujio wake katika kiota hicho.
Dj Bon Lov ambae ndo mpango mzima wa Fleva nite akiwa Bi. Kidude ambaye alifika kwenye kiota cha mzalendo pub katika libeneke zima na flava nite ili kutia baraka kwa vijana wake kina Bon Lov.kushoto ni mdau Dullah.




Nyomi la wadau likiduarika usiku wa kuamkia leo kwenye kiota cha maraha cha mzalendo pub ambacho kila jumamosi kinatema ngoma za zamani yanii oldskool za kukata na shoka chini ya usimamizi wa dj nambari 1 nchini Tanzania Dj Bonny LUV na Dj MackayPICHA KWA HISANI YA HAKI NGOWI



No comments:
Post a Comment