Ofisa Mtendaji wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Justin Geyve (kushoto) na Simon de Roy wa Kampuni ya Platinum, wakishiriki katika katika mashindano ya mbio za kutembea za KM 9 zilizoandaliwa na Rotary Club of Dar es Salaam, kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia miradi ya maji katika shule za Dar es Salaam. Mbio hizo ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi zilianzia na kumalizia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi, Dar es Salaam jana. Jumla ya sh. milioni 130 zilichangwa.TBL ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo.Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Kevin O'flaherty akiwa na mkewe katika mashindano ya mbio za kutembea za KM 9 zilizoandaliwa na Rotary Club of Dar es Salaam, kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia miradi ya maji katika shule za Dar es Salaam. Mbio hizo ambazo mgeni rasmi alikuwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi zilianzia na kumalizia katika viwanja vya bwalo la maofisa wa Polisi, Dar es Salaam jana.TBL ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mashindano hayo.
PICHA KWA HISANI YA FULL SHANGWE

No comments:
Post a Comment