Ni jioni kwa sasa niko Mbagala katika eneo linaloitwa Mbagala kwa Nyoka katika shule ya Msingi Juhudi hapa upigaji kura umemalizika hivi sasa linaendelea zoezi la kuhesabu kura, lakini pembeni kuna watu mbalimbali wamejikusanya ili kujua kinachoendelea. Inasemekana eneo hili ni ngome ya chama cha CUF hivyo Polisi wa usalama hasa kikosi cha FFU wako hapa wakihakikisha usalama unakuwepo kama unavyoona wakiwa katika gari lao huku wakiwa wamevalia mavazi rasmi kwa ajili ya kujikinga na vurugu zozote zinazoweza kutokea hata hivyo hali ni shwari kabisa pamoja na kwamba wakati fulani kulitokea rapsha kidogo lakini zikazimwa.
Wananchi wakiwa wamejikusanya kandokando ya majengo ya sgule ya msingi Juhudi ambapo ndiyo kuna vituo vya kupigia kura habari zaidi zitawajia baadae kadiri zitakavyopatikana kutoka katika maeneo mbalimbali ya uchaguzi.PICHA KWA HISANI YA FULL SHANGWE
No comments:
Post a Comment