ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 3, 2010

UCHAKACHUAJI ULIVYOLETA KIZAAZAA MWANZA!

FFU wakipambana na wafuasi wa chadema kwa kuwapiga mabomu ya
machozi jana majira ya sa 12 jioni

Kizaazaa mtaani!
Wafuasi waChadema wakidhibitiwa na polisi katika lango kuu la
halmashauri ya jiji ili kuepuka vurugu kutokea endapo wangeingia ndani ya uzio
wa ofisi hizo
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro aliwasihi wanachama na
wafuasi wa chadema kuwa watulivu kusubiri matokeo kutangazwa nyuma ni mgombea
ubunge jimbo la Nyamagana Ezekia Wenje na kulia kwa RPC ni mgombea udiwani
aliyeshinda Kata ya Kitangiri, Bw. Matata


RIPOTI KAMILI
Na Mashaka Baltazar,MWANZA 
SAKATA la Msimamizi wa uchaguzi katika majimbo ya uchaguzi wa Nyamagana na
Ilemela kuchelewesha kutangaza matokeo ya ubunge katika majimbo hayo jana
yaligeuza viunga vya jiji la Mwanza kuwa Bagdad kwa polisi kupiga mabomu ya
machozi

Hali hiyo ilitokana na wananchi wanaodaiwa kuwa wafuasi wa chama cha Demokrasia
(CHADEMA) kushindwa kuvumilia baada ya msimamizi wa uchaguzi jiji la Mwanza, Bw.
Wilson Kabwe kuchelewa kutangaza matokeo na kusababisha vurugu hizo kutokea


Gazeti hili lilishuhudia wafuasi hao wa chadema wakiwa wamefurika mbele ya lango
kuu la kuingia katika ofisi za msimamizi wa uchaguzi jiji tangu majira ya
asubuhi huku wakiimba nyimbo za kuhamasishana na kuwakandya CCM kuwa
inawakumbatia mafisadi.


Ilipofika majira ya saa 5:00 Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Simon Sirro
alifika katika ofisi za jiji kasha kuingia ndani na kukaa kw dakika kadhaa kabla
ya kutokan nje ambapo alifuatwa na mgo,bea wa xchadem,a jimbo la Nyamagana ,
Bw. Ezekia Wenje ambaye alimtaka haki iteteke kwa kumtanganza mshindi ili
kuepusha vurugu.

Hata hivyo kamanda huyo alisema kuwa hakuna vurugu zitakazotokea kwani jeshi la
polisi lipo kwa ajili ya kulinda usalama na limejipanga na kuwataka wafuasi wa
chadema kutovunja sheria kwa kigezo cha matojkeo kuchelewa kutangazwa.

Alisema hata baada ya mshindi kutanagzwa wanachama na wafuasi hao wa chadema
wasifanye maandamano kwa kuziba barabara , badala yake wapite pembeni na
kusherehekea ushindi kwa amani .

Aidha kitendo cha msimamizi kuambatana na wagombea ubunge wote wa chadema na
kuwaomba wafuasi wao wavumilie wakati mchakato wa kuhesabu kura na kuziweka
katika mfumo wa kielektroniki ukiendelea, klizidisha munkari kwa vijana hao.

wakizungumza na wafuasi wao kwa nyakati tofauti wagombea hao wa chadema Ezekia
Wenje (Nyamagana ) na Highness Samson Kiwia (Ilemela) waliwataka kuwa watulivu
na kuwahakikishia kuwa kura zao ziko salama na hakuna wa kuzichakachua na haki
yao itapatikana na kudai baada ya tratibu wangetangaziwa matokeo

Ilipofika majira ya saa 8:19 Msimamizi wa uchaguzi akiwa na pamoja na wagombea
aliwasihi wazungumze na wafuasi wao huku akiahidi kutangaza matokeo hayo baada
ya saa moja na nusu ambapo walikubali,muda huo tayari magari ya polisi
yakiongozwa na kikosi cha mbwa yaliwsili eneo hilo kuhakikisha usalama
unakuwepo.

Walitinga eneo hilo wakiwa katika magari matatu, moja likiwa lnye nama za
usajili STK 834 likiwa na askari wa kikosi cha mbwa watau, magari yenye namba PT
2063, PT 2492 yakiwa na askari 11 waliovalia mavazi maalum ya kupambana na
vurugu,.Pia gari la maji ya kuwasha nalo liliwasili hapo tayari kudhibiti vurugu
kama zingetokea.Muda huo ilikuwa ni majira ya saa 8:19 mchana.

Ilipofika majira ya saa 12:00 bila mtokeo kutangazwa wafuasi hao wa chadema
waliamua kufurumsha mawe na ndipo FFU walipojibu kwa kupiga mabomu ili
kuwasambaratisha wafuasi hao wa chadema na kusababisha vilio kusikika kila
mahali ndani ya ofisi za jiji na hata katika hospitali ya mkoa wa Mwanza Sekou
Toure .

Mabomu hayo yaliendelea kupigwa na kusababisha baadhi ya mitaa ya jiji na
barabara kufungwa, ambapo wafuasi hao walikwenda hadi nyumbani kwa Kabwe
wakitaka kuchoma moto nyumba yake.

Vurugu hizo hazikuishia hapo zilieendelera kwenda kumalizia hasira katika ofisi
ya CCM Kata ya Isamilo na kuichoma moto, ikiwemo baadhiya magari kuvunjwa vioo,
ambapo pia gari la RPC Sirro kukumbwa na dhoruba naada ya gari lke kupigwa mawe
vioo vyake.

Mwingine anayedaiwa kukumbwa na kadhia hiyo ni mwenye gari namba T 836 aca baada
ya kuchomwa moto .Hata hivyo wafuasi haop walirejea tena wakiashiria amani na
kusababisha polisi kushindwa kuwapiaga mabomu hadi matokeo yalitpotangazwa hyuku
polisi wakiwa wameondoka eneo hilo.

Awali kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, Bw.Simon Sirro alifika eneo hilo na
kukutana na umati wa wafuasi wa chadema wakiimba kushangilia ambapo aliingia
ndani ya ofisi za msimamizi wa uchaguzi na kuondoka kabla ya kufanya mazungumzo
mfupi na Bw.Wenje ambaye alilimlalamikia kuchelewesha kutangazwa kwa matokeo.


“Nawaomba muwe watulivu wakati kura zikiendelea kuhesabia na taratibu zingine
kufanyika, msifanye vurugu tulieni ili baadaye mshindi aangazwe na hatimaye
twende kusherehekea ushindi kwani kura zenu ziko salama hazijachakachuliwa”
alisema Bw.wenje na kufuatiwa na Bw. Highness Kiwia mgombea wa ubunge jimbo la
Ilemela ambaye naye aliwasihi wafasi wao kutulia na kusisitiza hakli yao ipo
kuna utaratibu ulikuwa ukifanyika ili washindi watangazwe.

Hata hivyo hali libadilika majira ya saa 7:45 ambapo afuasi hao wa chadema
waliamua kulitikisa lang kuu la ofsi za msimamizi wa uchuguzi kushinikiza
kuwatangaza washindi baada ya muda mrefu kupita hali iliyosababisha OCD
Nyamagana kushuka chini na wagomba hao wa chadem kuwataka wafuasi wao kuacha
fujo na wawe na subira kwani matokeo yangetangazwa baada ya saa 1:30 baada ya
zoezi kukamilika.


Kabla ya matokeo hayo kutangazwa kuliibuka madai kuwa msimamizi wa uchaguzi
alikuwa akishinikiza kumtangaza mshindi, mbunge wa CCM aliyemaliza muda wake Bw.
Lawrance Masha, huku mgombea wa CCM jimbo la Ilemela Bw. Athony Diallo akielezwa
kukubali kushindwa na wa chadema.

Kutokana na kuchelewa kutangazwa kwa washindi wa ubunge katika majimbo mawili ya
jiji la Mwanza, kulizuka uvumi kuwa waziri wa Mambo ya Ndani, ambaye alikuwa
mgombea wa CCM akitetea kiti chake alikuwa amelazwa kutokana na shinikizo la
damu uvumi ambao gazeti hili limethibitisha si kweli waziri huyo kalazwa.



Hko Ukerewe nako polisi waliazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya
wafuasi wa chadema majira ya saa 4:00 ambao walikuwa cwakishinikiwa msimamzi wa
jimbo hilo Leonard Masele kumtangaza mshindi wa cahdema Bw. Salvatory Machemli
dhidi ya mgombea wa CCM Getrude Mongella, ambapo baadaye Machemli alitangazwa
mshindi.
CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: