ANGALIA LIVE NEWS

Friday, November 12, 2010

Obama akutana na Jintao, Merkel katika G20


Rais Barack Obama katika mazungumzo na Rais wa China Hu Jintao kando ya mkutano wa G-20 mjini Seoul, Korea Kusini.

Rais Barack Obama katika mazungumzo na Rais wa China Hu Jintao kando ya mkutano wa G-20 mjini Seoul, Korea Kusini

Viongozi wa nchi za kundi la G20 watakutana Ijumaa kwa kikao cha mwisho cha mkutano wa G20 unaojumuisha nchi zenye uchumi ulioendelea na ule unaoinukia.

Alhamisi, Rais Barack Obama alifanya mazungumzo yaliyohusu maswala mengi na Rais wa China Hu Jintao na Chansella wa Ujerumani Angela Merkel. Katika taarifa fupi baada ya mkutano wao Rais Obama alisema Rais Hu hakusema lolote kuhusu mgogoro wao juu ya sera za sarafu ya China, swala kubwa katika uhusiano wa China na Marekani.
Rais Obama alisema Marekani na China zinaona maendeleo makubwa katika maswala mbali mbali kati yao, na zina wajibu mahsusi kuhakikisha ukuaji wa uchumi katika nchi zao. Rais Hu alisema China iko tayari kushirikiana na Marekani kuongeza mazungumzo na ushirikiano baina yao
                                        HABARI KWA HISANI YA VOA

No comments: