picha ni Samwel Sarakikya mwalimu wa Hisabati.
Picha hii imewekwa kama kielelezo cha habari hapo chini na Mwalimu Samweli Sarakikya sio mwalimu anaezungumziwa.
Teacher wa Shule ya Msingi Pemba, Edmund Kadudu iliyopo katika Kijiji cha Pemba, Wilaya ya Mvomero, Mkoa wa Morogoro, ameelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi wapatao 1,000 anaolazimika kuwafundisha kwa zamu kuanzia darasa la kwanza hadi
saba.
saba.
Mwalimu huyo ameomba msaada kutoka Halmashauri ya Wilaya hiyo kuweza kuongezewa walimu wengine ili kukabiliana na tatizo hilo lililodumu kwa zaidi ya miaka minne, imeelezwa.
Kwa mujibu wa mwalimu huyo, kuwa shule hiyo yenye wanafunzi zaidi ya 1,000 inakabiliwa
na uhaba mkubwa wa walimu ambapo kwa muhula ujao wa masomo huenda akaendelea kufundisha pekee kutokana na mwalimu mkuu wa shule kuonyesha mazingira ya kutaka kuhama.
Alisema hali hiyo itajitokeza kutokana na Mwalimu Mkuu kumweleza kuwa amepata uhamisho wa kwenda kufundisha shule moja ya msingi iliyopo mkoani Tanga.
“Tunalo tatizo la uhaba wa walimu …na si uhaba tu , shule haina walimu , tulikuwa walimu wawili kwa maana Mwalimu Mkuu, lakini amesema kuwa amepata uhamisho wa kwenda
Mkoa wa Tanga, hivyo muhula wa masomo utakapofunguliwa nitabakia pekee yangu,” alisema mwalimu huyo.Hata hivyo aliongeza kusema”
…Mwalimu Mkuu alikuwa akifundisha mara moja moja na kuondoka, hivyo kwa muda wa miaka minne nipo pekee yangu kuwafundisha wanafunzi, “alisisitiza Mwalimu huyo.
Akizungumza kwa huzuni na masikitiko makubwa, Mwalimu huyo alisema kuwa amekuwa akifundisha kwa zamu kuanzia darasa la kwanza hadi la saba na kwamba kutokana na wingi wa wanafunzi kazi ya ufundishaji imekuwa ngumu kwake.
Kwa mujibu wa Mwalimu huyo, kuwa darasa la pili lina wanafunzi 250 na wengine 600 ni wa madarasa ya tatu hadi sita, ambapo wataongezeka wengine wa darasa la kwanza mwakani na kufikisha idadi ya 950.
“Tatizo hapa ni uhaba wa walimu , wanafunzi wanavyo vipaji na wa kupata walimu wa kutosha shule inatoa wanafunzi wengi wa kuingia kidato cha kwanza,“ alisema Mwalimu
huyo.
CHANZO:DARHOTWIRE
Hivi kweli Serikali ipo serious!!!!!!
ReplyDelete