J e shemeji yako anaweza kua mshikaji wako??
Nilipokua Houston Jumamosi ilyoisha December 18,2010,katika mazungumzo kulitokea ubishi kuhusu shemeji ambae ni mume wa dada yako kama anaweza kuwa mshikaji?kwa maana ya kwamba mna hang out pamoja kama vile kwenda baa kupata moja moto moja baridi.
Ubishi huu ulikua mkubwa uliogawa makundi mawili ambayo kila moja lilitetea upande wake.
Kundi linalopinga kwamba mume wa dada yako hawezi kuwa rafiki yako kwa sababu kuu moja,"napotoka kwenda baa na washikaji mara nyingi tunazumgumzia wanawake na hii haimanishi tunaondoka nao,bali ni mazungumzo yakusaidia kutelemshia kilaji pia ni mazungumzo ya kawaida kwa washikaji wanapokutana.lakini mazungumzo kama hayo siwezi kuzungumza na shemeji yangu ndio maana shemeji atabaki shemeji hatakua rafiki yangu" na akaongezea na hata napokuja kuwatembelea sitalala nyumbani kwao nitakaa kwa mshikaji au Hotelini.
Kundi linalotetea shemeji kua mshikaji wao walikuja na sababu kwamba yote inategemea uhusiano ya wewe na dada yako ukoje,kama dada yako mna uhusiano ulioshikamana basi hata mume wake uhusiano utakua hivyo hivyo na wakaongzea kwa kutoa mfano wa kama shemeji yako anaishi ughaibuni na akakupa mchongo wa shule na akakulipia nauli ya kuja ughaibuni huwezi kufika huko ukakataa akutoe vumbi kwa kukupeleka huko na kule,je unafikiri atakuelewaje?
Kundi linalopinga shemeji kua mshikaji walipinga hoja hiyo kwa kusema kukubali huduma za shemeji yako si sahihi kwa maana atazarau ukoo wenu na siku akielemewa anaweza kumkimbia dada yako.
Je mdau wa Vijimambo unasemaje kuhusiana swala hili tupe maoni yako
yah inawezekana maana unaweza kukuta mshikaji. walikuwa marafiki kabla hajamuoa dada, kwa hiyo unaniambia kwa kuwa nimekuwa shemeji yako ushikaji uushie? maana unaona noma story za bar?
ReplyDeleteKimsingi, kwangu mimi nadhani awe alikuwa rafiki yako kabla ya kuoa dada yako au la, ukweli ni kwamba kwa kuoa dada yako tayari ameunga ukoo. Hivyo suala la kuwa naye karibu au kutokuwa naye karibu sio issue ya kuizungumzia. Kwenda naye baa si kigezo cha kujenga hoja. Nilidhani wangelizungumzia kuhusu kushirikiana kibiashara zaidi.
ReplyDeleteNinawafahamu jamaa wawili ambao wameoleana dada zao na ni wafanyabiashara wakubwa Kariakoo. Sina uhahikika unapozungumzia kudharauliwa katika uhusiano huu una maana gani. Akishakuwa shemeji yako ni ndugu yako, na kwamba maslahi yake ndio ya dada yako, na ya dada yako ndio yako. Kwa mtizamo huo uhusiano kwa kwenda naye bar sio hoja ya msingi ya kuijenga katika uhusiano huu.
Mnyalu
yaani hapa bonge la so,nachoona hapa ni kwa ukisha kuwa shemeji wa mtu sura inabadilika hapa inabidi heshima iwepo kama ulikuwa mshikaji basi yale mambo ya kuongoza kwanza yanapungua inategemea urafiki wenu ulikuwa wa namna gani kama ulikuwa wa kukutana kwenye kinywaji basi mmoja inabidi abadilishe viwanja na ninadhani wanaume wengi ambao hawajawa na wenyemba nyumba kamili ndiyo wana hizo za kusimulia mambo hayo na matokeo yake kama unatoka na dada yatu ujue ugomvi na mwenye nyumba wako utakuwa kila siku maana huyo shemeji yako atamuadithia dada yake jinsi ulivyo na hautaacha kutongonza sasa bado unachovyachovya tu na hi aibu pia kwa huyo shemeji.
ReplyDeleteNa kama ni shemeji yako amefikia hapo kwako basi msaidie usimpeleke kwenye anga zako na kama mmetoka kupata wape taarifa ni mgeni wangu jamani nadhani mtu ukiwa na mgeni wako mambo kama hayo ya hayatakiwi akisha kuwa mwenyeji nayeye atapata kundi lake sidhani kama niwote kila siku wanadicuss habari hizo tu jamani.
na kama umeenda kutembelea hao ndugu zako rasmi kwanini ufikie kwa rafikilabda sehemu iwe ndogo vinginevyo lala hata sebuleni.maana wewe ni mgeni nadhani hauchukui hata siku 10.jamani tuheshimiane na watu waache kupenda dezo ndiyo maana shemeji yako anaweza kukupeleka kwa vimada hiyo ni hishara kwa wewe na dada yako wote anawadharau