Kampuni ya Uingereza ya kutengeneza silaha, BAE Systems, imekiri hatia ya kutohifadhi taarifa sahihi kuhusu kuuzia Tanzania mtambo wa Radar uliogharimu dola bilioni arobaini.
Hatua ya BAE kukiri makosa hayo ni sehemu ya makubaliano baina yake na idara inayopambana na ufisadi ambapo BAE ilitakiwa kutoa majibu kuhusu kesi kadhaa za ufisadi.
Imeelezewa kuwa kampuni hiyo ya BAE Systems ilimteuwa raia wa Tanzania Shailesh Vithlani kama wakala wa kisiri wa kuisadia kupata zabuni ya kuiuzia Tanzania mtambo wa radar.
Wakala huyo alipelekewa malipo yake kupitia kampuni moja iliyosajikliwa katika visiwa vya British Virgin Islands huko Amerika ya kusini.
BAE Systems imekiri kwamba fedha hizo zilikusudiwa kumlipa kwa kazi aliyofanya ya kuishawishi serikali ya Tanzania kuipendelea kampuni hiyo katika kutoa zabuni.
Mahakama imeelezewa haingewezekana kubaini Bwana Vithlani alizitumia vipi fedha hizo.
Shirika la Uingereza linalohusika na kupambana na ufisadi limesema halitaishtaki kampuni ya BAE kwa rushwa , ila kwa kukosa kuhifadhi mahesabu sahihi ya biashara hiyo.
Hakimu Bean aliyesikiliza kesi hiyo amesema kampuni hiyo haikutaka kuhusishwa na fedha hizo.
Alisema BAE Systems haikutaka kujua ni kiasi gani cha pesa kilicholipwa wala nani aliyepokea malipo, na kwamba wao walichotaka ni kazi hiyo itekelezwe.
Kutokana na kukiri makosa hayo, BAE imesamehewa kesi zote za ufisadi zilizokuwa zinachunguzwa mkiwemo swala la kuiuzia silaha Saudi Arabia, Jamhuri ya Czech na Afrika Kusini.
BAE imesema imechukua hatua madhubuti kuhakikisha inatimiza maadili ya hali ya juu katika biashara.
Hukumu kamili itatolewa siku ya Jumanne.
No comments:
Post a Comment