ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 29, 2010

Bei ya gesi yazidi kupaa


Rais Jakaya Kikwete akikagua mtambo wa kufua umeme kwa njia ya Gesi, Badala gesi asilia kuwa chanzo cha kuleta unafuu kwa wananchi sasa nayo imeanza kupanda kwa kasi jambo linaloashiria kuanza kwa matumizi ya mkaa jambo ambalo ni hatari kwa mazingira.
Editha Majura
WAKATI Watanzania wakiendelea kutafakari namna watakavyokabiliana na ongezeko la gharama ya maisha kufuatia ongeza la bei ya umeme kwa asilimia 18.5, imebainika bei ya gesi ya kupikia imeongezeka kati ya Sh 4000 mpaka Sh9000 ndani ya kipindi cha miezi miwili.


Utafiti uliyofanywa na gazeti hili kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam, umebaini kuwa tangu mwezi Oktoba mpaka Desemba mwaka huu, bei hizo zimepanda kwa kasi  ambapo  mtungi wenye uzito wa kg 6 ulikuwa ukiuzwa Sh 16,000 kisha  Sh 18,000 na sasa unauzwa Sh 20,000.

Wenye uzito wa Kg 12 awali uliuzwa Sh 32,000 ukapanda mpaka kufikia Sh 36,000 sasa unauzwa Sh 39,000 huku wenye kg 12 ambao ulikuwa ukiuzwa Sh 37,000 kisha Sh 42,000 sasa unauzwa Sh 49,000.


Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Titus Kaguo, akizungumza na Mwananchi jana kuhusu suala hilo alisema gesi inazalishwa pamoja na nishati ya mafuta hivyo bei ya petrol inapopanda na bei ya gesi inapanda.
“Kweli bei ya gesi imepanda na ni jambo ambalo lipo nje ya uwezo wetu kwa sababu ni bidhaa ambayo bei yake inadhibitiwa kwenye bei za soko la dunia,” Kaguo alisema.
Kaguo alisema mwamko mdogo wa wafanyabiashara wa kuuza gesi nao unachangia kuongezeka kwa bei kwani wakiwa wachache wanaringa.

  “Tumeanza kutekeleza hatua za awali za kuhamasisha Wafanyabiashara wengi wauze gesi ili kuwapata  wengi na wauze kwa ushindani,” alieleza

                                                    Chanzo:Mwananchi

No comments: