Monday, December 13, 2010

Dk. Remmy Ongala enzi za uhai wake.
Mwanamuziki mkongwe nchini, Dk. Remmy Ongala amefariki dunia jijini Dar es Salaam leo.
Habari za awali zilizofikia mtandao huu zinasema Dk. Remmy alikata roho akiwa nyumbani kwake usiku saa nane na robo kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya kisukari.
Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na mipango ya mazishi bado haijajulikana
.
Wimbo wa Kifo aliouimba DK Remy miaka mingi iliyopita, bila shaka ndiyo utakaotamba katika kipindi hiki cha kifo chake na wakati wa maombolezo yake kutoka na uzito wa maudhui yaliyomo kwenye wimbo huo.


                      CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

1 comment:

  1. R.I.P.DOCTOR TUTAKUKUMBUKA KWA NYIMBO ZAKO ZOTE.MEYA SEATTLE WA

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake