Na Luqman Maloto
Memba mwenye ‘uzani’ mkubwa ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Zitto Zuberi Kabwe amelishwa sumu, ripoti ya daktari inafunuliwa na familia yake.

Zitto a.k.a Super Kabwe anayewakilisha Jimbo la Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya CHADEMA, alikula chakula chenye sumu lakini nafuu ni kwamba haikufika kwenye damu.
Habari kutoka kwa ndugu wa Zitto na kuthibitishwa na mama mzazi wa mbunge huyo, Shida Salum, zinasema kuwa vipimo vya daktari vinaonesha kuna chembechembe za sumu kwenye chakula alichotumia.
“Kwa kifupi majibu ya daktari yameonesha kuna chembechembe za sumu kwenye chakula alichokula,” alisema Mama Zitto na kuongeza:
“Daktari amesema labda chakula kilikuwa kichafu lakini ukweli ni huo kuwa kilikuwa na sumu, ila sumu hiyo haikufika kwenye damu. Tunamshukuru Mungu.”
Mama Zitto hakutaka kuzungumza kirefu kwa maelezo kwamba amebanwa na mkutano wa Kamati Kuu ya CHADEMA ambayo yeye ni mjumbe. Alisema: “Nipo kwenye kikao cha Kamati Kuu, Zitto hayupo, bado anaumwa.”
Kwa upande mwingine, ndugu wa mbunge huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake gazetini alisema, majibu ya daktari yanakamilisha kile ambacho wao kama familia walikuwa nacho.
Alisema, kwa namna ilivyotokea haikuwa rahisi kushindwa kutambua kuwa Zitto aliwekewa sumu kwenye chakula au ndani ya kinywaji alichotumia.
“Kuna vitu vingi vinaendelea hapa na hatujui ni nani aliyehusika na mchezo huu wa kumuwekea sumu kwa sababu ripoti ya daktari imesema ni food poison (chakula chenye sumu),” alisema ndugu huyo.
Aliendelea kusema: “Kama familia tunaliangalia hili na tupo tayari kumlinda kwa gharama yoyote. Haijapita wiki tumepata SMS ya watu wanaodaiwa kupanga njama za kummaliza, leo kalishwa sumu, haikubaliki.”
ZITTO ALIVYOANZA KUUGUA
Jumatano ya wiki iliyopita, Zitto alikuwa ni mmoja wa wabunge wa CHADEMA waliokuwepo kwenye semina ya siku mbili kwenye Hotel ya Palm Tree, Bagamoyo, Pwani.
Mchana, Zitto alijumuika na wabunge wenzake wa chama hicho kwenye chakula lakini jioni alihamia Hoteli ya Millennium mjini hapo kwenda kulala.
Wakati anaelekea Hoteli ya Millennium, alielezwa kuhusu tafrija ya wabunge wote (party) ambapo alitoa udhuru wa kutohudhuria kwa maelezo kwamba hakujisikia vizuri.
Saa saba alishikwa na ugonjwa wa tumbo, Mbunge wa Biharamuro Mashariki (CHADEMA), Anthony Gervas Mbassa ambaye kitaaluma ni daktari wa magonjwa ya binadamu, aliitwa kumpatia huduma ya kwanza.
Habari zinasema kuwa Mbassa alimpatia matibabu Zitto kwa siku nzima lakini kesho yake (Alhamisi) majira ya saa 11 jioni alikimbizwa Hospitali ya Aga Khan, Dar kwa matibabu zaidi.
Zitto, alilazwa Aga Khan kwa siku mbili na kuruhusiwa juzi (Jumamosi) majira ya saa sita adhuhuri.

MBUNGE ANAYEMSAPOTI NAYE HOI
Mbunge wa Mpanda Mjini CHADEMA, Said Amour Arfi ambaye anadaiwa kusapoti msimamo wa Zitto, naye yupo hoi na alitarajiwa kusafirishwa kwenda India kwa matibabu zaidi.
Arfi, alizungumza na mwandishi wetu Ijumaa iliyopita akiwa wodini kwake kwenye Hospitali ya Aga Khan kuwa anakwenda India kufanyiwa upasuaji baada ya kugundulika ana mawe tumboni.
Alisema: “Naondoka leo (Ijumaa iliyopita), ilikuwa nifanyiwe oparesheni leo hapa hapa Aga Khan lakini baada ya Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) kuja, akaamua nikafanyiwe oparesheni India.
“Alikuja pia hapa Spika wa Bunge (Anna Makinda), kwahiyo taratibu za safari zinafanywa na Wizara ya Afya, nitaondoka leo (Ijumaa iliyopita) jioni.”
Afri ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA taifa, ni mmoja wa wabunge ambao hawakuingia bungeni kuungana na wenzao ili wasusie kwa pamoja hotuba ya Rais Jakaya Kikwete.
Timu ya wabunge ambao hawakuingia kabisa bungeni, wanadaiwa kuwa upande wa Zitto.
CHADEMA SHEREHE
Wakati Zitto na Arfi wakiwa hoi, CHADEMA kwa nyakati tofauti walijumuika pamoja kwenye tafrija mbalimbali.
Sherehe ya kwanza ni ile iliyofanyika kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar ya kumpongeza mfanyabiashara Mustapha Sabodo kwa mchango wake kwenye chama hicho.
Kabla ya sherehe hiyo, wabunge walijumuika kwenye ‘pati’ maalum ambayo Zitto akiwa mzima alikataa kwenda na wakati wakiendelea ‘kula bata’, Afri alikuwa hoi Aga Khan.
NI SIKU MBILI BAADA YA SMS YA KIFO
Jumanne ya wiki iliyopita, gazeti ndugu na hili la Uwazi, liliripoti habari ya kuwepo kwa SMS inayodaiwa kuandikwa na kiongozi mmoja wa CHADEMA kwenda kwa viongozi wengine, inayoelekeza namna ya kumuua Zitto kijasusi.
SMS hiyo inasomeka: “Nawaarifu kwamba nipo Mara nimemaliza kukutana na viongozi wa Mwanza. Inaelekea hawakubaliani na hoja yetu ya kumfukuza Zitto, sasa nilikwisha kusema kwamba tuweke mkakati kwenye Media JF. Ni …, … na … (yanatajwa majina ya watu).”
SMS hiyo inaendelea: “Ni …, … na … (majina mengine ya makada wa CHADEMA) watatekeleza kazi tuliyowapa na … (anatajwa kiongozi wa CHADEMA) atawapa mtu wa kuwaongezea nguvu.”
Ujumbe huo hauishii hapo, unaendelea: “Kuweni makini, hakikisheni amewapa nyaraka zote alizonazo kabla ya kumuua, usiri unahitajika, … atawasaidia kujua nyendo zake na hii tu ndiyo njia ya kukinusuru chama.”
Miaka minne iliyopita, Zitto aliwekewa sumu kwenye maziwa katika hoteli moja jijini Mwanza na kuokolewa na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM), marehemu Amina Chifupa ambaye alimpigia simu na kumueleza asiendelee kunywa.
Amina alimueleza Zitto kuwa maziwa hayo yalikuwa na sumu lakini kwa sababu alishakunywa mengi, dakika chache baadaye aliishiwa nguvu na kukimbizwa kwenye hospitali moja jijini humo ambapo alipatiwa matibabu.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS
Jamani kweli Tanzania tumefikia hivi? Hizo hoteli zimechukuliwa hatua gani? Maana hii si shughuli iliyofanyika nyumbani kwa mtu its in a hotel for god's sake! This means hii mission iliwahusisha wapishi? maserver or what? Please tupeni ufaffanuzi how could this happen.
ReplyDeleteMtanzania mkereketwa
POLE SANA MHE..ZITTO NA POLENI MAASIDI WAKE SIKU YAKO YA MAAUTI BADO NI MNWENYEZI MUNGU TU AJUAE...KWA KWELI THIRD WORLD COUNTRIES TUNAMATATIZO.........MEYA SEATTLE WA
ReplyDeleteHajalishwa sumu bwana daktari kasema ni Food poisoning watanzania wanatafsiri amelishwa sumu. Kaazi kweli kweli. Food poisoning sio kulishwa sumu jamani.
ReplyDelete