Show ya "Growing Up African" inayo onesha familia kutoka Tanzania na maisha yao Marekani imeanza kutoa video. Kwenye mwezi huu wa December kila wiki kutuakua na Episode zitazokuja kwenye website yao. Episode ya kwanza inaonekana sasa hivi na tunawaomba watanzania wenzetu waangalie hizi episode hili
show iingie kwenye network haswa. Kwenye hizi episode utakutana na ndugu wote kwenye familia kutoka kwa Bea, Eliza, Jesca, Johnson hadi Andrew amabo huwa maisha yao ni tufauti kwa kila mtu. Episode nyingine zitakuwa na familia nzima ambao utaona hile "family dynamic" ya ndungu. Hapo hapo kutakuwa na vipindi kama PSquare kwenye New York City, na arusi kubwa ya ndugu na mambo ya mengi hili watanzania waone maisha yalivyo Marekani.
Kutakua kuna mambo ya kitanzania kila saa kama Party ilivyokua, Washington DC ya Uhuru wa Tanzania na Speech ya Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda alivyofika hapa New York kwenye Delegation. Hii show kwanza, niyasisi Watanzania na tunabidi tuwasikie mnavyosema kabla ya kuwa kwenye International Spotlight na network kubwa huku Marekani.
Watu hizo episode wanaweza kwenda kwenye youtube.com, bongo5.com au G5click.com kwenye "Growing Up African kuona hayo mambo. Website saa hivi hiko tayari na yenyewe ina mambo mengi sana kama mawazo ya familia kwenye issues kama musiki, fashion, urembo, na vinginevyo vingi kwenye blog zao.
Mwezi wa December utakuwa Introduction ya mambo ya show na bado tunaendelea kusikiliza maoni ya watu huko nyumbani na ndio familia itachagua network ya kuirusha Season ya kwanza. Familia itakuja Tanzania mwakani, 2011.
Asanteni Sana, na ninaomba ushauri na mawazo kutoka kwenu kama watanzania wenzetu.
Kwa mwenye ushauri zaidi naomba ujisikie huru kuwasiliana nami kwa
Cellphone: +1917 442 1822
Barua Pepe: lupembejames@yahoo.com
James Lupembe
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake