Dardanus(Kushoto) ni shabiki wa Simba na Hadji Helper ni Yanga damu
Hadji Saidia au Hadji Helper na Dardanus Mfalme ni marafiki toka enzi hizo wanapiga “chandimu” pamoja mitaa ya Kinondoni.Ila kwa sasa jamaa hawa wanaishi kwenye states tofauti hapa Marekani.Hadji yupo Atlanta na Dardanus kalikita Houston.Jamaa hawa walianzisha some kinda vita ndani ya Facebook,vita vyao sio vya matusi au comments zisizo na vichwa wala miguu bali ni kwenye fani ya kughani mashairi.Personally,nadhani it was fun to read them hasa kwa kuwa wote ni washkaji zangu.
Well,cheki shairi hili toka kwa Dardanus kujibu shairi la Hadji Helper:
SHEHE HADJI vs MFALME… Jibu 2
Popo karuka mchana, taya zimewadondoka,
Hamjawahi kuona, hata mapenzi ya paka,
Vipi mwataka shindana, na dafu nyie vidaka,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Popo karuka mchana, taya zimewadondoka,
Hamjawahi kuona, hata mapenzi ya paka,
Vipi mwataka shindana, na dafu nyie vidaka,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Walianza malumbano, ya tungo na mashairi,
Ulikuwa mvutano, nusu ugeuke shari,
Shehe kapewa kibano, akaanza kughairi,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Ulikuwa mvutano, nusu ugeuke shari,
Shehe kapewa kibano, akaanza kughairi,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Kuja kwenye danadana, KINGI akapiga mia,
Shehe kajaribu sana, sitini hakufikia,
Mwishoni akala kona, swaumu ‘lipomjia,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Shehe kajaribu sana, sitini hakufikia,
Mwishoni akala kona, swaumu ‘lipomjia,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
KINGUNGE ni mlokole, kwa wewe usiyejua,
Na tena bado mpole, mwenye Roho kama hua,
BICCO alitoka kule, MUNGU kumtumikia,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Na tena bado mpole, mwenye Roho kama hua,
BICCO alitoka kule, MUNGU kumtumikia,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Ujanja wote wa SHEHE, kapata kwa MFALME,
Akitaka starehe, video akatazame,
Mpira hata sherehe, Mwasi Klabu akazame,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Akitaka starehe, video akatazame,
Mpira hata sherehe, Mwasi Klabu akazame,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Hebu SHEHE mwulizeni, mkimwona hivi leo,
Kwa mara ya kwanza lini, alitazama video,
Kwani yote Kinondoni, ni KINGI mwenye kideo,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Kwa mara ya kwanza lini, alitazama video,
Kwani yote Kinondoni, ni KINGI mwenye kideo,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Tukija kwenye kabumbu, KINGI kafunika tena,
Yupo kwenye kumbukumbu, UMISETA alifana,
SHEHE HADJI kama nyumbu, butua butu kwa sana,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Yupo kwenye kumbukumbu, UMISETA alifana,
SHEHE HADJI kama nyumbu, butua butu kwa sana,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Aheri ya Mkoloma, alicheza Kibasila,
Ingawa anakoroma, boli kwake limelala,
Moshi akaja kusoma, tukacheza bila hila,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Ingawa anakoroma, boli kwake limelala,
Moshi akaja kusoma, tukacheza bila hila,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
SHEHE maji ya ugoko, kwa MFALME nasema,
Zake zote chokochoko, kwa KINGI zimetuama,
Kawekwa kwenye mfuko, hafurukuti daima,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Zake zote chokochoko, kwa KINGI zimetuama,
Kawekwa kwenye mfuko, hafurukuti daima,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI.
Wadau mnaosoma, nisomeni kwa makini,
KINGUNGE nimesimama, nashika nambari wani,
SHEHE HADJI anazama, inamwelemea fani,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI
KINGUNGE nimesimama, nashika nambari wani,
SHEHE HADJI anazama, inamwelemea fani,
MKALI ni MFALME, KINGUNGE wa KINONDONI
CHANZO:TUNYFISH
No comments:
Post a Comment