Thursday, December 16, 2010

MAREHEMU DK. REMMY ONGALA AAGWA BIAFRA, DAR

Familia ya Ongala ikiwa wakiwa katika viwanja ikifuatilia taratibu mbalimbali za tukio hilo.

MAELFU ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam walijitokeza mchana huu kuuaga mwili wa mwanamuziki Remmy Ongala katika viwanja vya Biafra, Kinondoni, jijini Dar es Salaam kabla ya kuzikwa jioni ya leo.  Ongala aliyekuwa mwanamuziki maarufu nchini, alifariki mwanzoni mwa juma hili katika Hospitali ya Regency jijini Dar es Salaam ambako alikuwa akitibiwa.
Kally Ongala, mmoja wa watoto wa Ongala akiwa amekaa kwa huzuni kubwa
Wanakwaya waliokuwa wanasali na marehemu Ongala wakiimba wimbo wa kumsifu mwenzao aliyewatoka.
Waziri wa Utamaduni, Habari na Michezo, John Nchimbi, akimpa mkono wa pole mjane wa marehemu.
Nchimbi akisaini kitabu cha maombolezo
Jeneza lililobeba mwili wa marehemu
Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azzan, akisaini kitabu cha maombolezo.
Msanii wa maigizo, Bakari Mbelemba (Mzee Janngala) akifuatilia matukio uwanjani hapo.Wanafamilia wa marehemu wakipita mbele ya jeneza.

                               PICHA: ISSA MNALLY/GPL

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake