
Stuart Holden (shoto) wa Bolton Wanderers akijaribu kuzuia mashambulizi ya Ramires (kulia) wa Chelsea katika mechi za Barclays Premier League kati ya Chelsea na Bolton Wanderers iliyochezewa uwanja wa Stamford Bridge December 29, 2010 London, Uingereza ambapo Chelsea waliibuka washindi kwa 1-0.

Florent Malouda (shoto) wa Chelsea akikung'uta kigongo kimo cha mbuzi huku Jussi Jaaskelainen golikipa wa Bolton Wanderers akijaribu kuokoa bila mafanikio.

Florent Malouda (shoto) wa Chelsea akishangilia bao safi pasi kutoka kwa Didier Drogba

Florent Malouda (kulia) wa Chelsea akipongezana na mchezaji mwenzake Ramires (shoto) baada ya kupachika bao safi.
No comments:
Post a Comment