ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 14, 2010

Mwakilishi wa Marekani Afghanistan na Pakistan afariki dunia.


Richard Holbrooke, mwakilishi maalum wa Marekani Afghanistan na Pakistan.
Richard Holbrooke enzi za uhai wake
Mwanadiplomasia wa Marekani Richard Holbrooke  amefariki dunia.
Hivi karibuni alifanyiwa upasuaji wa kurekebisha tatizo kwenye mshipa  mkubwa wa moyo.

Holbrooke ambaye alikuwa akifanya kazi na utawala wa Obama kama mwakilishi maalum wa Pakistan na Afghanistan  aliugua ghafla Ijumaa wakati wa mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton .
Alikimbizwa hospitali na kufanyiwa upasuaji kwa saa 20 ambao ulifuatiwa na  upasuaji mwingine mdogo Jumapili.
Clinton amesema salaam zimekuwa zikimiminika kutoka duniani kote.  Rais wa Afghanistan Hamid Karzai na wa Pakistan Asif Ali Zardari ni kati ya walioonyeshwa kuguswa.
Rais wa Marekani, Barack  Obama alimuita Holbrooke, ambaye alikuwa na umri wa miaka 69 kuwa ni mnara katika sera za mambo ya nje za marekani. Miongoni mwa mafanikio yake makubwa ilikuwa ni jukumu lake katika mashauriano ya  mikataba ya amani iliyojulikana kama 1995 Dayton Peace Accords  ambayo ilimaliza vita vya Bosnia – Herzegovina.
                                                    CHANZO:VOA

No comments: