ANGALIA LIVE NEWS

Monday, December 13, 2010

Mwenzi wako anatoa harufu mbaya? Soma ujue jinsi ya ‘kuinjoi’ naye

Usafi ni msamiati mgumu katika mapenzi. Utafiti unaonesha kwamba ipo sehemu ya wanaume na wanawake ambao huamua kusaliti ndoa au uhusiano wao kwa sababu ya kuudhiwa na vionjo vya faragha.


Usafi ni kionjo murua katika mapenzi. Wewe kwa jinsi ulivyo, utajiongezea alama za ziada kwa mwenzi wako endapo utakuwa huna kasoro zinazosababishwa na uchafu kila mnapokutana faragha.

Wapo watu ambao walilowea kwa watu wa pembeni baada ya kuchoshwa na uchafu wa wenzi wao. Wanasema uchafu wa nyumba hukimbiza wageni, hivyo mwenzi wako mpya kama mgeni, anapokutana na kero ya uchafu, atakukumbia.

Hata hivyo, mada hii ina lengo la kuwafanya watu wawe bora kwenye mapenzi. Watulie na wenzi wao kwa namna inayotakiwa. Hoja hii ipewe nafasi kwamba kuachana, kwa namna fulani inaweza kuifanya jamii ikuone una matatizo hata kama mwenzio ndiye mwenye matatizo.

AINA YA UCHAFU
Kuna uchafu wa nguo! Kwa maana mtu unaweka viwalo mwilini ambavyo havina muonekano sahihi. Mtu hata akikaa mbali na wewe kwa mita tatu, haimfanyi ashindwe kugundua kwamba mavazi uliyovaa yamechafuka. 

Aibu!Usafi wa nguo za ndani! Nimewahi kuzungumza kwamba mtu anavaa ‘kufuli’ mpaka mwenyewe anajionea aibu. Wakati anapoingia faragha na mwenzi wake, anajibana kuvua mpaka aombe taa izimwe. Hii ni kujidhalilisha.

Tunapomzungumzia mwanaume, wapo wanaoamini kuwa usafi kwao si muhimu. Wanaamini wanawake peke yao ndiyo wanaowajibika katika kujiweka wasafi. Matokeo yake ‘kufuli’ moja inavaliwa mwezi mmoja. Wanahitaji msaada wa kitaalamu.

Mwanamke anaposhindwa kuwa maridadi. Mbali na kufuli ya chini, pia anatinga ‘bra’ kwa maana ya sidiria ambayo hata haisomeki rangi yake. Tuelekezane kwamba usafi uende sambamba na ulinzi wa rangi halisi za nguo husika.

Katika hili, nifafanue kwamba kuna watu ambao kwa kutothamini unyeti wa nguo za ndani, huamua kuloweka kwenye maji, wanapitisha sabuni kisha wanatupia kwenye kamba au kitu chochote cha kuanikia pasipo kuhakikisha kwamba nguo yenyewe imetakata.

Hapo kuna kosa kwa sababu athari yake huonekana baada ya kufua mara mbili. Ile rangi yake kamili haitoonekana, badala yake kitakuja kitu tofauti. Kufuli nyeupe itakuwa ya rangi ya udongo, huku sehemu yenye jasho ikigeuka nyeusi. Hili lisifanyiwe mchezo. 

Lipo kundi hili! Nguo ya ndani sijui mtu anakuwa nayo moja au makusudi. Anaingia kuoga, halafu anafua kabati yake, kitu ambacho ni kizuri. Lakini anakosea kwa sababu huivaa kabla haijakauka. Kuna hatari kubwa kwenye hili.

Mtu anapovaa nguo ambayo haijakauka, hasa ile ya ndani, husababisha harufu mbaya mfano wa kitu kilichovunda. Hapo ni busara kwako kujiuliza kama unaona ni sahihi kwako uwe unanuka mfano wa muhogo mbichi uliolazwa kwenye maji wiki nzima. Kataa aibu hii!

Mbali na kunuka, ipo hatari kwako ya kupata maradhi. Wataalamu wa ngozi wanasema kuwa mtu anapovaa nguo mbichi, yupo kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa fangasi. Chukua hatua haraka!

Kuna uchafu wa chumba! Unatakiwa ulale kwenye sehemu nadhifu kila siku. Ukimkaribisha mwenzi wako, ajidai. Isiwe kuna nguo zimetupwa bila mpangilio, hewa chafu mpaka upumuaji unakuwa si mzuri. Hewa safi ndani ya chumba ni afya.

Usafi wa nywele! Tunajua hizo za juu, ni kweli kwamba wapo watu ambao ni wavivu kuzihudumia. Wanaume wengine hutaka kufuga au kushindwa kuzinyoa mpaka kusababisha ziwe kero kwa mtu atakayekuwa karibu yake.

Harufu!Hili kwa wanawake ni zito mno, kwa maana wao ndiyo mara nyingi husuka lakini kwa sababu ya kushindwa kuzihudumia, husababisha zitoe harufu mbaya ambayo huwa kero kwa mwenzi wake wanapokutana faragha.

Zipo nywele za kwapa na za kule sirini zaidi! Hayo ni maeneo ambayo hutafsiriwa kwamba hutoa jasho lenye mafuta, kwa maana hiyo yasipohudumiwa ipasavyo, hutoa harufu kali ambayo inaweza kumkimbiza yeyote kukaa jirani na wewe.

Ni uchambuzi tu wa usafi, unachotakiwa ni kutoogopa kwa sababu kuna dawa nitakupa ambayo itakuwezesha kudumu na mwenzi wako ambaye anasumbuliwa na tatizo la harufu. Muhimu ni kuhakikisha hukosi nakala yako ya Ijumaa Wikienda toleo linalokuja.

No comments: