Na Mwandishi Wetu
Pamoja na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mganga maarufu wa Tiba Asilia, Mheshimiwa Steven Ngonyani ‘Profesa Maji Marefu’ amesema hawezi kuacha kazi hiyo ya uganga.
Pamoja na kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), mganga maarufu wa Tiba Asilia, Mheshimiwa Steven Ngonyani ‘Profesa Maji Marefu’ amesema hawezi kuacha kazi hiyo ya uganga.
Prof. Maji Marefu aliyechaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi uliofanyika Oktoba 31, mwaka huu, alikaririwa akiyasema hayo hivi karibuni na gazeti moja litokalo kila siku.
“Ubunge ni dhamana iliyokuja nikiwa mganga wa tiba asilia, sasa nikisema niache nitakuwa siitendei haki dhamira yangu na wateja wangu,” alisema Mheshimiwa huyo.
Alisema kuwa alianza kuguswa na masuala ya siasa mwaka 1995 baada ya kuteuliwa kuwa meneja wa kampeni wa aliyekuwa mgombea na baadaye Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM), Laus Mhina.
Aliweka kweupe kwamba, tofauti na siasa, mambo ya tiba asilia alikuwa nayo hata kabla ya ‘kubatizwa’ uprofesa wa masuala hayo mwaka 1989 nchini Nigeria hivyo hawezi kuyaacha.
Kwa mujibu wa watu wanajua tiba asilia, kazi hiyo ni kama uchawi hivyo kumtafsiri Prof Maji Marefu tofauti na wabunge wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Prof. Maji Marefu ni mbunge mwenye historia ndefu ikiwa ni pamoja na kuzunguka ndani na nje ya nchi kwa kazi hiyo ya uganga huku makao yake makuu yakiwa wilayani Lushoto, Tanga.
CHANZO:GPL
1 comment:
safi sana. kwanini uache kazi yako bwana. kwani walivyokuchagua hawakujua kama wewe ni mganga wa kienyeji? fanya unachotakiwa kufanya..
Post a Comment