ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 30, 2010

Serikali 'yawavutia pumzi' wageni kuajiriwa kiholela

NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga
Mwandishi Wetu
NAIBU Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga, mapungufu yaliyoko katika sheria za kazi hapa nchini, yanasababisha baadhi ya kampuni binafsi, kuajiri watu wageni hata kwa kazi zinazostahili  kufanywa na Watanzania.

Dk Mahanga aliyasema hayo juzi kufuatia hoja iliyowasilishwa na Ofisa Kazi wa Mkoa wa Mara,Venance Kadago, ambaye alisema idara yake imekuwa ikifanya ukaguzi katika kampuni binafsi na kukuta wafanyakazi wa kigeni walioajiriwa kwa mikataba ya muda mfupi bila kuwa na vibali kutoka Wizara ya Kazi.

Ofisa huyo alisema vibali wanavyopewa wageni ili kuwaruhusu kuishi nchini, vinatoa mwanya kwa watu hao, kufanya kazi ambazo vinginevyo, zinaweza kufanywa na Watanzania.

"Mapungufu yaliyoko katika sheria ya sasa ndiyo yanayosababisha matatizo haya yote. Maofisa uhamiaji huko mikoani, wamekuwa wakitoa vibali vya kuwaruhusu wageni kuishi nchin," alisema Dk Mahanga.
Alisema kwa kutambua tatizo hilo, wizara yake inaandaa marekebisho ya sheria za kazi, itakayoainisha vizuri majukumu ya wizara katika kutoa vibali vya kazi na majukumu ya maofisa uhamiaji katika kutoa vibali vya wageni kuishi nchini.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa mwingiliano na mgongano wa majukumu ya wizara na uhamiaji.

Dk Mahanga alikuwa akizungumza na wafanyakazi wa wizara hiyo wa Mkoa wa Mara ambapo alisema pamoja na utandawazi na nchi kuingia kwenye ushirikiano wa kikanda wa kiuchumi, biashara na ajira, si vyema kuruhusu  kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania, kufanywa na wageni.


                                                      Chanzo:mwananchi
Alitumia mwanya huo kutoa rai kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Idara ya Uhamiaji, kushirikisha na wizara yake, kushughulikia matatizo yanayohusu ajira kwa wageni hata kama sheria bado zina mapungufu.

No comments: