Nawakaribisha watanzania wote waishio Washington DC Metro(DMV) katika mkutano wangu wa kwanza rasmi na watanzania.
Madhumuni ya mkutano huo yatakuwa yafuatayo:-
(i) Balozi kujitambulisha rasmi kwa Watanzania washio katika eneo la Washington DC Metro.
(ii) Kuchagua na kuunda kamati ya muda itakayoandaa katiba mpya ya jumuiya na hatimaye kuitisha na kusimamia uchaguzi mkuu wa Jumuiya mpya ya watanzania waishio Washington DC Metro.
(iii) Masuala mengineyo muhimu yatakayojitokeza yanayohusu watanzania waishio hapa Washington DC Metro.
TAREHE:
Januari 29, 2011
MAHALI:
Hollywood Ballroom - 2126 Industrial Pkwy, Silver Spring-MD 20906
(Sehemu ya maegesho ipo yakutosha)
MUDA:
Saa 10.30 jioni (Tafadhali zingatia muda)
Ili kukamilisha maandalizi ya mkutano huo, unaombwa kujiandikisha Ubalozini kwakuandika jina lako hapa chini.Sehemu hii ni salama(secure)nataarifa zako zitalindwa.
Maelezo yako ni kwa lengo la kufanikisha mkutano huo nakujenga takwimu kuhusu Diaspora ya Watanzania. Taarifa zote zitahifadhiwa kwa siri.
Ahsanteni.
Mwanaidi Sinare Maajar
BALOZI
kwa kujiandikisha Bofya Hapa
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake