WAZIRI wa Mawasiliano,Sayansi na Teknolojia,Profesa Makame Mbarawa amewashukia watendaji wa Shirika la Posta nchini(TPC) kwa kukosa ubunifu jambo ambalo limesababisha kushindwa kuingia kwenye soko la ushindani wa kibiashara kama zilivyo kampuni zingine.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa kampuni zinazofanya shughuli za posta ambayo mengi yao yanafanya kazi vizuri katika sokohilo.
Mbarawa alisema kuwa kuingia kwenye soko hilo lazima menejimenti ya utawala ipange mikakati ya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora za posta, jambo ambalo litawafanya wananchi walitumie shirika hilo.
Mbarawa alisema kuwa kuingia kwenye soko hilo lazima menejimenti ya utawala ipange mikakati ya kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora za posta, jambo ambalo litawafanya wananchi walitumie shirika hilo.
“Lazima muingie kwenye soko la ushindani ikiwa ni pamoja na kuwa wabunifu wa shughuli zenu na kuangalia utaratibu mzuri wa kusafirisha vifurushi kwa wakati jambo ambalo litasaidia wananchi kupenda kutumia huduma yenu,”alisema Profesa Mbarawa.
Aliongeza kutokana na hali hiyo menejimenti inapaswa kutumia huduma mbalimbali ambazo zinatumiwa na kampuni zingine kwa ajili ya kutoa huduma hiyo katika maeneo yote ndani na nje ya nchi.
Alisema, mpaka sasa TPC imeshindwa kutoa huduma ya Posta ambayo inatumika katika nchi nyingi za Afrika na Ulaya kutokana na kukosekana kwa ubunifu huo.
Alibinisha kutokana na hali hiyo shirika hilo linapaswa kutoa huduma mbalimbali za posta ili liweze kukidhi mahitaji.
Naye Posta Masta Mkuu wa TPC, Deous Mndeme alisema kuwa, tangu kuvunjwa kwa shirika la Posta na Simu nchini, shirika hilo limeweza kujiendesha kifaida ikilinganishwa na miaka iliyopita.
Alisema , kutokana na hali hiyo wanahitaji kiasi cha Sh30.7 bilioni kwa ajili ya kuboresha huduma za uendeshaji ndani na nje ya nchi.
“Tunahitaji kiasi cha Sh30.7 bilioni ili tuweze kujiendesha kibiashara, hii inatokana na kuhitaji Sh32bilioni kwa ajili ya kufufua majengo yetu na kuwekeza katika mipango mbalimbali ya kazi yetu, wakati Sh7.7 bilioni kwa ajili ya kujiendesha kibiashara,”alisema Mndeme.
No comments:
Post a Comment