ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 30, 2010

HARAMBEE,COLUMBUS,OH,JUMAMOSI,OCT,2,2010

Mr. Matthew Salukele (Marehemu)

kutakua na harambee ya marehemu Mzee Matthew Salukele Jumamosi Oct 2,2010 saa 11 jioni(5:00pm)

Worthington Activity Center
909 Proprietors Road,
Worthington,OH,43085

Tunaombwa tujitokeze kwa wingi ili tuweze kusaidia kusafirisha mwili wa marehemu mpendwa Mzee wetu Tanzania,kufiwa hakuna mmoja,leo ni Happy na David, kesho ni mimi na wewe,na ndugu wa karibu wa Happy na David ni Mimi na Wewe,laiti kifo kingekua kinatoa taarifa yote haya yasingetokea lakini yote haya tumwachie Mwenyezi Mungu kwani ni Yeye anaetoa na kutwaa na Jina lake litukuzwe.

Unaweza pia kusaidia kupitia Chase Bank Acc #917118267 Routing # 044000037.

Msiba upo Add: 
1427 hideaway Woods Dr
Westerville OH 43081

Tunatanguliza Shukrani kwa msaada wako

For more information Please contact:
David Salukele cell# 614-859-9602
Walter kalosi cell#614-537-1448
Happiness Salukele  cell#614-772-5126
Adella Njau cell#614-446-9710
Dorah Njau cell#614-589-5685
Jacqueline Mjengwa Cell# 614-804-5237 

experienced coaches/players needed


Attn: 
INTRODUCTION 
Ref: EC/GOCN/EXP/VOL.II/05 
http://www.lifanfc.com
 
The CHONGQING 
LIFAN FOOTBALL CLUB intends to invite experienced coaches/players/expatriate capable of rendering expertise services the chinese national team and there clubs in the chinese supper league divison.their enthusiasm fed by huge media coverage. 
 
BASIC FUNCTION: 
To coach and provide leadership instruction to the chinese national team. 
 
CHARACTERISTIC DUTIES AND RESPONSIBILITIES
*Development of team strategies; analyze performance of 
football team and adjust strategies as needed. 
*Coordinate team travel arrangements. 
*Scouting and recruiting more players into the national team. 
*Coordinate coaches clinic; supervise 
dress code for staff and team members. 
 
MINIMUM QUALIFICATIONS
: 
Education and 
Experience
Bachelor
閳ユ獨 degree in relevant field, 
 
SALARY: US$29,000.00, Monthly, can be transferred to any Bank or Country of your choice and all transfers must be made in conformity with the existing tax situation in 
China . 
 
CONTRACT DURATION
: 48 months (Liable for upward review depending on your commitment and expertise) 
 
MODE OF EMPLOYMENT

The Management hereby inform that you are to INCUR all expenses associated with the processing of your relevant papers for commencement of work.
 
The chinese football association will disburse Six (6) months Upfront salaries and relocation expenses on confirmation of your required documentation (including immigration papers) from the relevant authorities here in China 
 
We hereby inform that if this Offer is acceptable to you, you are requested to send us an
acceptance letter with your passport photograph via email to:koshimaee35@yahoo.com.cn, and your C.V/RESUME to enable us proceed with relevant processing. 
 
We await your response in this regard. 
Regards 
 
Mr   Koshi Maee
CHONGQING LIFAN FOOTBALL CLUB
No.52 international Park Xiang Gang Zhong ,Liaocheng,
Shandong Province CHINA 252000

GENEVIEVE AKABITHIWA BENDERA YA TAIFA

Genevive Emmanuel akiwa ameshikilia bendera ya taifa mara baada ya kukabidhiwa rasmi tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China leo.
Vodacom Miss Tanzania, Genevieve Emmanuel Mpangala, jana ikabidhiwa Bendera ya Taifa tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China katika jiji la Sanya ambako shindano la dunia Miss World 2010 inatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu. Genevieve ataondoka leo kwa ndege ya Shirika la Quatar Airways akipitia Uarabuni, Mongolia na kisha kutua Sanya nchini China. 
Esther Mkwizu (wa pili kushoto), ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi na aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi Bendera ya Taifa kwa Vodacom Miss Tanzania akikabidhi bendera hiyo huku wazazi wa Genevive wakishuhudia, kulia ni baba yake Bw. Emmanuel Mpangala na kushoto ni mama yake Mary.
picha kwa hisani ya GPL

Mpenzi wako anahisi unamsaliti, huna mapenzi ya dhati kwake, ufanyeje?

Wiki iliyopita nilizungumzia suala la kumsoma mpenzi wako na kujua anahitaji nini kutoka kwako kisha kumtimizia. Naweza kusema ni makala iliyoonekana kuwagusa wengi kwani nimepokea sms na simu nyingi kutoka kwenu mkinipongeza juu ya elimu hiyo niliyowapa. Nimefarijika sana!

Wiki hii nataka kuzungumzia suala la wapenzi wakati mwingine kufikiriana tofauti kiasi cha kusababisha hali fulani ya kupungua kwa mapenzi au kuachana.

Haya yanatokea sana na kama wewe hujawahi kukutana nayo basi rafiki au ndugu zako yanawakuta. Yapo mazingira ambayo huwafanya wapenzi kufikiriana tofauti, nitayaainisha kwa uchache kisha mwisho nitashauri cha kufanya.

Katika mawasiliano
Kwa kipindi hiki simu za mkononi zimekuwa ni chanzo kikubwa cha wapenzi kufikiriana tofauti. Yawezekana wewe ni msichana na una mazoea ya kupenda kuwasiliana na wanaume kwa mambo mengine yasiyo ya kimapenzi na hata kwenye simu yako kuna namba nyingi za wanaume.

Kama una mpenzi mwenye wivu ni dhahiri ushakutana na hali fulani ya mpenzi wako kuhisi kuwa hujatulia na una wanaume wengine, kiasi cha kumfanya ahisi yeye unamzuga tu.

Yawezekana kwenye ‘facebook’ yako una marafiki wengi wa kiume na hata unapokuwa ‘online’ hupenda kuchati nao tena katika mambo ambayo hayana maana. Unadhani mpenzi wako akikufikiria tofauti atakuwa anakosea? 

Kwa swali hili najua wapo watakaosema hakuna tatizo lolote endapo msichana atakuwa na marafiki wengi wa kiume na kupenda kuwasiliana nao. Ukweli ni kwamba, kama tujuavyo kwamba mapenzi ya kweli lazima yaende sambamba na wivu, ni sahihi mpenzi wako kukufikiria tofauti na wewe utakuwa na jukumu la kumhakikishia kuwa hakuna lolote linaloendelea kati yako na marafiki hao wa kiume.

Swali ni je,mpenzi wako atakuamini? Hudhani kwamba kwa kufanya hivyo utakuwa unamfanya ahisi unamsaliti? Kwanini uwe na marafiki wengi wa kiume ambao wanamfanya mpenzi wako akufikirie tofauti? 
Mimi nadhani katika hili kama nilivyosema wiki iliyopita, ukishamsoma mpenzi wako na kubaini kuwa hataki ujiweke karibu na wanaume bila sababu za msingi, jaribu kuanza kuwapotezea kiana ili umpe imani mpenzi wako.

Muwapo faragha
Eneo lingine ambalo linaweza kumfanya mpenzi wako ahisi humpendi ama unamsaliti ni kutoonesha furaha unapokuwa naye faragha. Mpenzi wako anajua kwamba wewe sio goigoi, anajua mapigo yako lakini sasa yawezekana kadiri siku zinavyokwenda badala ya kuongeza mahaba unapunguza na wala yale mambo yako yalee siku hizi mpenzi wako hayapati, kwanini asikufikie tofauti?

Mimi nadhani yapo mazingira mengi ambayo yanaweza kumfanya mpenzi wako ahisi humpendi au unamsaliti. Hakuna sababu ya kuyataja yote lakini kikubwa ni namna ya kumfanya asikuhisi hivyo. 
Kuna kila sababu ya kuhakikisha unaiondoa dhana hiyo kwani madhara yake ni kumfanya naye aanze kukusaliti au kupunguza mapenzi kwako na hatimaye kukuacha.

Yawezekana mpenzi wao anahisi humpendi au una mtu mwingine kutokana na ‘ubize’ wako wa kazi. Ni jukumu lako kumfanya aamini kwamba ni kweli kushindwa kwenu kuonana mara kwa mara kunatokana na kazi na sio sababu nyingine. Ukishindwa kumfanya aamini hivyo, atakuwa sahihi kuhisi unamsaliti au ndiyo unamuacha kimtindo, kwanini? Kwasababu siku hizi wengi hutumia janja hiyo, mpenzi wake ana hamu ya kuonana naye, anamwambia yuko bize?Utakuwa ni ubize gani huo ambao mpenzi wako haujui?

Huenda kutokana na kazi zako una ukaribu sana na watu wa jinsia tofauti, mfanye mpenzi wako aamini kwamba hao unaowasiliana nao mara kwa mara ni kutokana na asili ya kazi yako na wala hakuna suala la mapenzi. Kama ni muelewa atakuelewa kuliko kuendelea kutumia muda mwingi kuongea na wasichana tena mbele ya mpenzi wako na kuishia kusema ni marafiki tu, ni lazima atakufikiria tofauti.

Jamani nafasi ni ndogo lakini naamini mmeambulia kitu. Tambueni tu kwamba kumpata mtu mwenye mapenzi ya dhati kwako kwa kipindi hiki ni adimu sana hivyo ukibahatika katika hilo, hakikisha unalilinda penzi lako kwa gharama yoyote. Usikubali marafiki wasiokuwa na mpango wakuharibie uhusiano wako. Mfanye mpenzi wako akuamini hata unapokuwa mbali ili na yeye afanye hivyo hivyo!

Tukutane tena wiki ijayo.

INASIKITISHA SANA!


Hakika kifo hakina huruma, hakina saa wala notisi.Kilichomtokea mzee huyu leo asubuhi pale Ubungo Bus Terminal kinasikitisha sana. Mzee wa watu, ametoka nyumbani kwake asubuhi na mapema kuelekea kwenye kituo cha mabasi kwenda huko alikokuwa amepanga kuwa mgeni au kureja nyumbani kwake siku ya leo, bila kujua kuwa Mungu amempangia kifo chake leo kabla ya jua kuchomoza. Mzee, huyu ambaye hakutambulika mara moja, amegongwa na basi la abiria liendalo mikoani wakati likitoka lango kuu kwenda na safari zake, tairi lilipanda mwilini mwa mzee huyu na kumuua hapohapo akiwa ameshika mkoba wake wa safari mkononi. Hivi sasa tunavyosoma habari hii ya kusikitisha mwili wake uko mochwari katika hospitali ya Mwananyamala na kwa yeyote anayemfahamu ajitokeze, nahisi familia yake haina taarifa. Mungu alitoa na YEYE ametwaa mja wake, YEYE ndiye Mfalme wa Mbingu na Ardhi na KWAKE sote tutarejea!! Ailaze roho ya Marehemu Peponi - ameen!
umati wa wasafiri na wapita njia wakishuhudia mzee wa watu akiwa hana kauli tena
...basi la kushoto (ambalo halikuweza kujulikana mara moja) ndilo lililohusika na ajali hiyo. Dereva wake alijisalimisha mikononi mwa polisi, ingawa basi liliruhusiwa kuendelea na safari zake.
..askari polisi wakisaidiana na raia kumpakia marehemu garini
...maiti ikipelekwa kuhifadhiwa Mwananyamala hospitali.

PICHA: Mpiga Picha Wetu,na kwa hisani ya GPL

Wednesday, September 29, 2010

Colonel Maganga na Mkewe Washerehekea Miaka 25 ya ndoa yao,MD Sept 28,2010

Kanisa kama linavyojieleza hapo juu ambalo Colonel Emmanuel Maganga na Mkewe Love Maganga walisherehekea Miaka 25 ya ndoa yao
Colonel Maganga na Mkewe wakiwa na wapambe wao Prof Boas na Mkewe
Colonel Emmanuel Maganga na Mkewe Love Maganga wakivishana pete kama ishara ya Upendo wa miaka 25 ya ndoa yao
Colonel Maganga na Mkewe wakiwa wenye furaha baada ya kuvishana pete 
Colonel Emmanuel Maganga na Mkewe Love Maganga wakiwa pamoja na familia akiwemo Prof Boas 

Duh hii imekaaje???

SOKA MAREKANI KUITANGAZA TANZANIA


Pichani ni Rais wa Soccer , Patrick Steenberge.
Chuo Kikuu cha Drake cha Marekani na Chuo cha CONADEIP cha Mexico wanatarajiwa kutangaza mpira wa Marekani Mei mwakani utakaofahamika kama Kilimanjaro Bowl, kwa sababu Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye maeneo ya kihistoria na utalii. Rais wa Global Soccer, Patrick Steenberge, amesema leo kuwa Mei 17, 2011 kutakuwa na matukio mawili likiwemo la kliniki ya mchezo huo itakayofanyika mkoani Kilimanjaro na kuzuru zaidi ya robo ya vivutio vya kitalii ikiwamo Mlima Kilimanjaro.Steenberge alisema Mei 21 timu za vyuo hivyo zitamenyana kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika na Stadi za Biashara (MUCCOB’s), kabla ya kutembelea vituo vya yatima.Naye Kaimu Ofisa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Devota Mdachi, alisema ujio wa timu hizo utaitangaza Tanzania katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya michezo na utalii
Habari kwa hisani ya Swahilivilla.blogspot.com.

Nick Cannon Asks Corporate Sponsors to Pay for Birthday Bash

2010 Operation Smile Annual Gala
Actor Nick Cannon attends the 2010 Operation Smile annual gala at Cipriani, Wall Street on May 6, 2010 in New York City. (Getty Images)more pics »Nick Cannon (Getty Images)Nick Cannon recently sent out a mass email asking corporate sponsors to pay for his 30th birthday parties in New York and Los Angeles next month.

Boasting that confirmed guests include Beyonce Knowlesand her husband Jay-Z, Demi Moore and her husbandAshton Kutcher, Will Smith and Jamie Foxx, the actor has promised any companies who assist with the celebrations -- which are to be hosted by his wife Mariah Carey -- will receive tweets and exclusive photographs in recognition of their donation.

The email, sent by the star’s representatives and obtained by the New York Postnewspaper, said: “This is an extremely exciting opportunity to sponsor a fun and lavish event… opportunities range from gift bags and signage to tweets and photo ops.”

In return for a $2,500 donation, sponsors will feature in the gift bag, while a more generous $15,000 will guarantee “one tweet,” plus a “mention in all public relations materials.”

Additionally, those prepared to fork out the full $25,000 will earn the donator the official title of “host sponsor,” which includes “three tweets,” a “right to service out photos” and a “logo on all collateral.”

The couple are well-known for their love of lavish parties. To celebrate his wife’s 39th birthday, Nick whisked Mariah -- who is worth an estimated $400 million -- off to the Caribbean island of Barbados for an exclusive celebration.
Image
Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa (katikati) akisalimiana na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum wakati mgombea huyo alipokutana na viongozi mbalimbali wa dini Dar es Salaam jana. Kushoto ni mgombea mwenza, Said Mzee Said. (Picha na Fadhili Akida).

Uokoaji wa Marekani waisha vibaya

Mashua nyepesi
Takriban watu 13 walizama na wengine wanane hawajulikani walipo baada ya manowari ya kijeshi ya Marekani yalipojaribu kusaidia mashua nyepesi ndogo tena nyembamba iliyoharibika kwenye ghuba ya Aden.
Maafisa wa manowari hayo ya kijeshi mjini Washington walisema USS Winston Churchill ilijaribu lakini ilishindwa kurekebisha injini ya mashua hayo mepesi.
Ikaanza tena kuyavuta manowari hayo pwani ya Somalia.
Lakini jitihada za uokoaji zilibadilika na kuwa balaa wakati abiria walipokimbilia upande mmoja wa chombo hicho kupata chakula na misaada, na kusababishia ipinduke.
Abiria wote 85 walirushwa kwenye maji, japo wengi wao waliokolewa.
Jeshi hilo la majini la Marekani lilikuwa na Waethiopia 75 na Wasomali 10, na boti hiyo ilikuwa ikitokea Somalia.

Uchunguzi

Boti hiyo mwanzo iligunduliwa katika ghuba ya Aden siku ya Jumapili.
Baada ya mabaharia kutoka kwenye manowari kushindwa kurekebisha injini ya mashua hayo madogo, walianza kukivuta chombo hicho pwani ya Somalia.
Abiria 61 waliokolewa na kwa sasa wako kwenye meli ya USS Churchill, lakini 13 walizama na wanane hawajulikani walipo.
Jeshi hilo lilisema bado linafanya uchunguzi kujua kitu gani kilitokea.
Haijajulikana wazi kwanini mashua hayo yalikuwepo eneo hilo, njia inayopita meli nyingi iliyokumbwa na mashambulio na maharamia wa Kisomali.
Lakini Umoja wa Mataifa umesema takriban Waafrika 74,000- zaidi kutoka Ethiopia na Somalia- walivuka ghuba ya Aden kuelekea Yemen mwaka 2009 wakikimbia umaskini na migogoro.

Hatimae Mwali Atua,Saranac Club

Timu kapteni wa Stars United(kandanda safi kiwango cha TBS) Libe Mwang'ombe akiwa na kombe waliochukua Atlanta,GA,kwenye mashindano ya Bongo soccer flava 2010 yaliyoshirikisha timu nne,Tanzanite ambo ni wenyeji,Alabama,Houston na Mabingwa wa mashindano hayo Stars United

Dangulo La Kienyeji Labainika Masaki Jijini Dar






HUKU Serikali ya Tanzania kkwa kushirikiana na jumuiya za taasisi kupambana na magonjwa ya Ukimwi lakini hali imekea tofauti ambapo hapo jana Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Oyster-Bay kwa kushirikiana na kikosoi maalum cha Polisi Jamii kubaini danguro linalotumiwa kwa ajiliya kufanyia biashara ya ngono.

Kubainika kwa danguro hilo la kienyeji ni kufuatia msako mkali uliofanywa na Mwenyekiti wa mtaa huo Peter Mushi kwa kushirikiana na kikosi hicho cha Polisi Jamii kijulikanacho kama ‘Oyster Bay Guard’ ambapo walifanya msako huo mkali nakubaini danguro hilo kubwa linalotumiwa na kwa biashara hiyo ya ngono zembe kwa makahaba hao huku likiwa na uwezo wa kuingiza watu saba kwa wakati mmoja.
Mwenyekiti huyo akiwa ameongozana na waandishi walifika katika eneo hilo ambalo lipo mkabala na ukumbi maalufu wa burudani katika barabara ya Haile Selasie na Quba, huku mmiliki anayelitumia kwa kufanyia biashara ya kupanda na kuuza miche na maua mbalimbali, inadaiwa ameligeuza eneo hilo majirta ya jioni kwa biashara hiyo.
Mushi aliwaelezea waandishi wa habari kuwa, zoezi kubwa lililopo katika mtaa wake huo ni juu ya kuwaondoa wafanyabiashara hao wa ukahaba sambambanakutokomeza uhalifu unaofanywa kwa kuiba kutumia magari.
“Zoezi ili litaendelea siku zote katika maeneio yote ya Oyster-Bay na kwa kuakikishabiashara hii ya ukahaba inaondoka na kuwa historia sambamba nakutokomeza vitendo vyote vya kiharifu maeneo haya ambayo yanaishi viongozi na maofisa wa nchi mbalimbali” alisema.
Kwa upande wake, mmiliki wa eneo hilo,alijitambulisha kwa jina moja la Mwinuko, alikana kwa eneo lake hilo pamoja na mashimo hayo kutumiwa kwa vitendo hivyo vya kikahaba huku akisisitiza kuwa makahaba hao wanapatumia hapo kwa manufaa yao wala yeye ausiki nao.
Eneo hilo ambalo kipindi cha nyuma lilikuwa maalufu kwa biashara hiyo huku makahaba hao wakiwabuguzi baadhi ya viongozi akiwemo kiongozi wa ngazi ya juu Serikalini kusimamishwa na kufanyia fujo katika eneo hilo la Oyster Bay.

HABARI KWA HISANI YA FULL SHANGWE

Lipumba aongoza kuharibikiwa magari

Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akizungumza na wananchi waliohudhuria moja ya mikutano yake.
Na Mwandishi Wetu
Katika Wagombea Urais wa Jamhuri Muungano wa Tanzania, watatu ndiyo wanapewa nafasi kubwa kutokana na mtaji wa kisiasa walionao lakini mmoja wao anatia fora kwa kuzimikiwa na magari.

Tathmini ya Risasi Mchanganyiko, ina majibu kuwa tangu kuanza kwa kampeni za kisiasa kwa wanaowania Urais, Ubunge na Udiwani Agosti 20, 2010, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Ibrahim Lipumba ndiye anakabilikiwa na matukio ya kuharibikiwa na magari katika mikutano yake kuliko wengine.

Lipumba ambaye ni mmoja kati ya Wagombea Urais watatu wenye nguvu, amewahi kuharibikiwa na magari mara mbili na matukio hayo kuripotiwa na vyombo vya habari, wakati alipokwenda kwenye ziara za kuomba kura kwa wananchi mikoa ya kusini.

Wakati kwa Lipumba ikiwa hivyo, kwa wagombea wengine wawili waliosalia wenye nguvu, Rais Jakaya Kikwete (CCM) na Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), wamekuwa wakiendesha kampeni zao kwa raha mustarehe pasipo bughudha.

Hata hivyo, uchunguzi wa Risasi umebaini kuwa kikubwa ambacho kinawafanya Slaa na Kikwete kutokumbwa na matukio hayo ni aina ya usafiri wanaoutumia ambao una tofauti kubwa na ule wa Lipumba.

Slaa na Kikwete wamekuwa wapasua anga kwa kutumia helkopta, isipokuwa katika maeneo machache, wakati Lipumba yeye usafiri wake muda mwingi ni wa gari, hivyo kukumbwa na masahibu hayo.
Ubovu wa barabara ni pointi nyingine ambayo imemfanya Lipumba akumbwe na misukosuko ya kukwama njiani, hivyo kuchelewa kuwafikia wapigakura wake.

Pamoja na hali hiyo, Risasi lilizungumza na baadhi ya wananchi ambao walimshauri Lipumba kufikiria upya kutumia usafiri wa helkopta ili kuendana na kasi ya wenzake.

“CUF ni chama kikubwa kuliko CHADEMA, kinapokea ruzuku nyingi kuliko CHADEM, hii inashangaza kinashindwa kuwa na ubunifu wa kufanya kampeni kwa helkopta wakati CHADEMA kimeweza. Kingine hata magari, kinatakiwa kuangalia yale magari yenye ubora,” alishauri mkazi wa Mwenye, Jamal Hamdun.

Mwananchi mwingine, mkazi wa Sinza, Anna Douglas alisema: “Isifikiriwe kwamba kutumia helkopta ni ufisadi, badala yake ionekane hiyo ni njia ya kusaidia kuwafikia wananchi kwa urahisi. 

Lipumba ana rekodi ya kugombea Urais tangu mwaka 1995, kwahiyo uzoefu wake ungemsaidia kujua kwamba usafiri wa anga hasa helkopta ni muhimu kwa kipindi hiki kwa sababu gari peke yake litasababisha maeneo mengi asifike.”
Chanzo:Global Publishers