Advertisements

Sunday, January 23, 2011

Balozi mpya,Jengo Jipya,mwaka mpya na mambo mapya



Mh.Mwanaidi Sinare Maajar
Jengo Jipya La Ubalozi Wetu,Washington,DC

Na Projestus Rwegarulila

Napenda kutoa shukrani zangu kwa ubalozi wetu hapo Washington DC. Kwanza kabisa tangia nilipofika hapa nchini mwaka 2003 nimekuwa nikisikia baadhi ya watanzania waishio
 Washington DC Metro wakilalamikia utendaji wa Maofisa hapo ubalozini kwetu jambo ambalo nilijaribu kulifuatilia kwa ukaribu kabisa na kugundua kwamba ni kweli kulikuwa na baadhi ya watanzania wenzetu ambao wamepewa dhamana ya kuitangaza nchi yetu huku ugenini pamoja na kushirikiana na watanzania waishio hapa kwa maslahi ya nchi yetu,lakini kwa namna moja au nyingine hawakutoa huduma hiyo katika standard ambayo ni ya kuwakilisha nchi ugenini na hasa hapa ambako ni mboni ya dunia.

Mungu kasikia kilio chetu na sasa tunao viongozi wetu wachapa kazi tupu wakiongozwa na balozi wetu mpya mheshimiwa MWANAIDI SINARE MAAJAR.katika jengo jipya lenye hadhi ya kimataifa.
Kwa ushuhuda tu nataka niwatangazie watanzania wenzangu kwamba mambo ni mapya na huduma pale ubalozini mambo ni mswano tupu.Nikianzia pale front desk,mpaka juu kwa Balozi mwenyewe
.
Mfano: Nilipiga simu tu kwa ofisa mmojawapo aitwaye bwana Suleiman afisa kwa mambo ya utalii nikamweleza jinsi ambavyo niko katika nafasi ya kutangaza nchi nikawa namshirikisha shughuli nzima huku ALABAMA. Siku iliyofuata alinitumia vifaa vya kuitangaza nchi kwa kutumia FEDEX kitu ambacho kisingewezekana siku za nyuma.
Na hata baadhi ya wanajeshi wanaosafiri kwenda Tanzania wamenipa ushuhuda kwamba utendaji wa maofisa wanaoshughulikia VISA wanafanya kazi nzuri na hapo nilijua tu kitakuwa ni kitengo cha bwana Abbas Abeid Missana.
Mifano hii naomba iwaoshe mioyo wale waliokuwa wamekata tamaa na ubalozi wao,kwamba washirikiane na ubalozi wao katika huduma mpya chini ya usimamizi wa balozi wetu mpendwa na maafisa wote kwa ujumla.
Naomba angalia video hii

3 comments:

Anonymous said...

Thanks Projestus. Hiyo inaonyesha jinsi gani mambo yamebadilika Ubalozini kwetu. Tunashukuru kwa ushuhuda. RJ

Anonymous said...

Kaka hupo Alabama sehemu gani, mimi nasoma hapa Alabama, JM

projestus rwegarulila said...

tufahamiane bwana unaitwa nani.mimi naitwa Projestus rwegarulila