ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, January 5, 2011

Viongozi wa CHADEMA wala kibano na kutiwa ndani Arusha.

Imeripoti kwamba katibu mkuu wa CHADEMA, DR. Wilbrod Slaa pamoja na mbunge wa jimbo la moshi mjini, MH. Philemon Ndesamburo wamekamatwa na polisi mkoani arusha usiku huu kwa madai kuwa na wao wamechochea vurugu zilizotokea leo mkoani humo. Viongozi hao wameungana na viongozi wengine waliokamatwa mapema leo kutokana vurugu zilizotokea wakati wa maandamano yaliyokuwa yakifanyika mkoani arusha leo.
Inasemekana kuwa viongozi wengine waliotiwa mbaroni hadi hizi sasa ni mwenyekiti wa chama hicho, MH. Freeman mbowe na mbunge wa jimbo la Arusha MH. Godbless Lema.

Tutawaletea habari zaidi pindi zikipatikana.

 





Mke wa Katibu Mkuu wa Chama cha CHADEMA Dk.Wilbroad Slaa, Josephine akiwa ametapakaa damu baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kipigo na polisi wakati wakivunja maandamano ya viongozi na wanachama wa chama hicho yaliyofanyika mjini Arusha jana.Katika maandamano hayo watu kadhaa walijeruhiwa baada ya kupigwa na pilisi wa kutuliza ghasia.Picha kwa msaada wa Mdau Paul Sarwatt ,Khalfan Said na Aravind BK

Bonyeza read more kwa habari zaidi.



















Viongozi wa juu wa CHADEMA, wakiongowa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe (Watano kulia) na katibu mku, Dk.Wilbroad Slaa(Wasita kulia) wakiongoza maandamano yaliopigwa marufuku na polisi jana mjini Arusha.Hatimaye polisi iliwatolea uvivu na kuwapiga kwa mabomu ya machozi. Habari zaidi zaeleza kuwa Mbowe anashikiliwa na polisi.
























Kasheshe zaidi


Picha kwa hisani ya: Hakingowi na Jiachie.

3 comments:

Anonymous said...

Chadema mie ni shabiki wenu mkubwa, lakini kuna mambo mnayoyafanya hayana maana. mnawapeleka wananchi kibao haswa wa hali ya chini kwenye matatizo badala ya kuwasaidia. Wameumizwa leo nyie mtaenda kujitibu wao watabaki kuhangaikia hela za matibabu. CCM wajanja wanatumia udhaifu wenu kufanya mabadiliko majimboni mwao( mfano Mh Makalla, kapeleka maji jimboni kwake, mawaziri wanafanya kazi kwa kishindo) N.K. sasa nyie sijaona hata badiliko mlilofanya toka mpate hizo nafasi zenu zaidi ya kubwabwaja na kutafuta mvunjiko wa amani kinguvu. SASA HICHO NDICHO TULICHO WACHAGULIA????? Fanyeni kazi acheni kubabaisha na kuchukua mishahara bure. bunge lipo pelekeni hoja. sio kila siku kampeni. TUMEWACHOKA SASA. NA KURA BORA TUWAPIGIE HAO HAO CCM. TATIZO LENU NYIE MNATAKA KUKIMBIA WAKATI HATA KUKAA HAMJAANZA. wenzetu wako mbali. Fanyeni mabaliko ya ukweli kwa wananchi waliowachagua na mtafika mnapotaka.ME NAWAONEA HURUMA WANANCHI MAANA KUMBUKENI ARUSHA NI MJI WA KITALII NA KUNA WANANCHI WANATEGEMEA KULA KUPITIA UTALII, LEO MNAENDA KUSABABISHA VURUGU AMBAZO MLISHAKATAZWA.
MDAU MAREKANI

Anonymous said...

wee mdau wa marekani my GRITS, nadhani unachemsha sisiemu ndio bado wamekaa wenyenchi tumeanza kukimbia toka miaka ya tisini, sasa wanatulazimisha sisi tukae tuu wakati wa kukimbia wanataka tukimbize mwenge wa nyerere (mtakatifu) mbio za mwenge zinaanza kutupa nuru baada ya miaka 49 za giza la nyerere its called blowback, i mean kiss my grits

Anonymous said...

NAFIKIRI NJIA BORA YA KUTULIZA VURUGU INAHITAJIKA ZAIDI KULIKO HIYO INAYOTUMIWA NA POLISI HUWEZI KUENDESHA NCHI KWA VITISHO NA VIPIGO UKADHANI UTAKAA KWA AMANI PENGINI NI KWA MUDA TU ILA WAKATI WAKO UTAFIKA MAANA DAMU ZA WATU SIO MAJI ZINALIA KWA UCHUNGU. MAMBO YALITOKEA KENYA NAYAONA YAKIJA KWA NGUVU NA HAKUNA ATAKAYE WEZA KUYAZUIA. WATCH OUT.