ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 19, 2011

Amri ya kutotoka nje yatolewa na Gbagbo-BBC

Maafisa nchini Ivory Coast wametoa amri ya kutotoka nje kwa kipindi cha siku tatu kote nchini kufuatia mpango wa maandamano yanayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa juma hili.
Tangazo hilo limejiri baada ya wafuasi wa Alassane Ouattara, mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha upinzani katika uchaguzi wa mwaka uliopita kuitisha mapinduzi ya kiraia kama yaliyotokea nchini Misri.
Bwana Ouattara anatambuliwa na jamii ya kimataifa kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi wa urais lakini rais wa sasa, Laurent Gbagbo, amekataa kuondoka madarakani.

Mteja wa benki akionyesha noti mpya.
Benki za mataifa ya kigeni zimearisha shughuli zake nchini Ivory Coast lakini bwana Gbagbo ametishia kuzitaifisha.
Mauzo katika mataifa ya ng'ambo ya zao la coacoa ambalo hukuzwa nchini humo kwa wingi yamepigwa marufuku na Ivory Coast inakabiliwa na tishio la kutumbukia katika mgogoro wa kiuchumi kama ule ulioshuhudiwa nchini Zimbabwe.

No comments: