Katibu wa muda wa habari na uenezi akitoa nasaha zake
Mwanachama mpya Drew akipokea kadi
Viongozi
Da Zainab akiwa na Misso Temu
Katibu wa muda akitoa nasaha zake
Katika sherehe za kuazimamisha miaka 34 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ,zilizo fanyika Siku tarehe 5, February 2011, Katika jiji la Houston, TX.Uongozi wa muda wa Tawi la CCM-MAREKANI unafuraha ya kuwatangazia wapenzi na wanachama wake wote ufunguzi wa shina Jipya la HOUSTON NO. 1; shina hilo lilichagua viongozi wao wakiwemo ,mwenyekiti Cassius Pambamaji na katibu Shaibu Said.Pia katika sherehe hiyo Tawi lilifanikiwa kuandikisha wanachama wengine wapya kumi na wawili.Pia ungozi wa Muda wa Tawi unapenda kuchukua nafasi hii kuutangaza uongozi wao ambao utakuwa madarakani kwa siku 120 toka ulipochaguliwa tarehe 2, January 2011.Viongozi hao wa muda ni kama wafuatao;
Novatus Simaba-Mwenyekiti
Abdallah Nyangasa-Katibu
Salum Rajab-Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi
Misso Temu-Kaitbu wa Uchumi na Fedha.
Kazi ya uongozi huu ni kuandaa na kuweka mazingira mazuri ya uchaguzi wa viongozi wa Tawi.
kwa picha zaidi tembelea blog yetu http://ccmmarekani.blogspot. com/
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Salum Rajabu,
Katibu wa Itikadi, Siasa na Uenezi,
Tawi la CCM-MAREKANI
USA




No comments:
Post a Comment