Timu ya Yanga jana imeshindwa kufurukuta dhidi ya Dedebit ya Ethiopia pale ilipokubali kipigo cha bao 2 bila majibu,mechi hii iliyochezwa Ethiopia ilikuwa ya marudiano,ile ya kwanza iliyochezewa Tanzania wiki mbili zilipita,Yanga iliambulia sare ya 4-4 dhidi ya timu hiyo(picha kwa hisani ya Full Shangwe)
YANGA jana iliaga michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Dedebit ya Ethiopia katika mechi ya marudiano iliyofanyika mjini Addis Ababa.
Kwa matokeo hayo, Yanga inakuwa imeaga michuano hiyo kwa jumla ya mabao 6-4 kutokana na kutoka sare ya mabao 4-4 katika mechi ya kwanza iliyofanyika Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Yanga iliyofika Ethiopia mapema Ijumaa na kudaiwa kufanyiwa vitendo visivyo vya kiuanamichezo ilitakiwa kushinda ama kutoka sare ya mabao 5-5 ndio ifuzu hatua inayofuata ya michuano hiyo.

Ushindi huo, Dedebit sasa itacheza na Haras El hadoud ya Misri katika mechi ya raundi ya kwanza.
Kwa mujibu wa habari kutoka kwa Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu aliyekuwa Ethiopia, bao la kwanza lilifungwa kipindi cha kwanza na lile la pili lilifungwa kipindi cha pili.
Sendeu alisema mchezo ulikuwa mzuri na pande zote zilikuwa zikishambuliana kwa zamu.
“Ndio hivyo mechi imekwisha na tumetolewa kwenye mashindano, tunasikitika kwa hilo sasa tunajipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani,” alisema.
“Wapinzani wetu hawakuwa wabaya kama wengi walivyodhani, huku tumekutana na upinzani mkubwa sana, wachezaji wao wamecheza vizuri na mechi ilikuwa kali mno kila upande ulikuwa ukifika langoni kwa mwenzie,” alisema.
Yanga imepata kipigo hicho ikiwa na kocha mpya, Mganda Sam Timbe aliyeichukua timu kutoka kwa Mserbia Kostadin Papic ambaye aliamua kubwaga manyanga baada ya kutofautiana na uongozi.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika siku chache baada ya Papic kubwaga manyanga ,Yanga ilikuwa chini ya kocha msaidizi Fredy Minziro.
No comments:
Post a Comment