Baadhi ya waombolezaji waliofika kuipokea miili ya ndugu zao wakiitambua kabla ya kutolewa ndani ya gari.
MIILI ya wanamuziki wa bendi ya taarabu ya Five Star Morden Taarabu waliofariki katika ajali ya gari eneo la Mikumi, Morogoro wakati wakitokea Mbeya, iliwasili jijini Dar es Salaam jana usiku majira ya saa moja na nusu kutoka Morogoro ilikokuwa imehifadhiwa hospitalini.
Miili hiyo ilipokewa makao makuu ya bendi hiyo katika ukumbi wa baa ya Equator uliopo Mtoni kwa Azizi Ally ambapo kulikuwa na umati mkubwa wa waombolezaji ambapo ilikabidhiwa kwa jamaa husika usiku huo huo.

Mwenyekiti wa bendi hiyo, Hamis Slim (kushoto), akilia kwa uchungu.

Umati wa waombolezaji uliojitokeza kuipokea miili hiyo.

Magari yakiwa yameziba Barabara ya Kilwa kuisubiri miili hiyo.

Mwili wa Issa Omary Kijoti ukichukuliwa na ndugu na jamaa.

Ndugu wa marehemu Husna Mapande wakiuchukua mwili wake.

Mbunge wa Tabora, Othuman Juma Kapuya (aliyekaa kulia), akiisubiri miili hiyo.

Waziri wa Michezo, John Nchimbi (kulia), akiiangalia miili ikiteremshwa kutoka garini.
( PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)
No comments:
Post a Comment