ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 5, 2011

Mpambano wa Yanga na Simba

Mchezaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi akijaribu kumpita beki wa Yanga kwenye mpambano uliochezwa leo uwanja wa Taifa ambato timu zote zimetoka suluhu ya bao 1-1,Yanga ndio ilikua ya kwanza kupata bao la penati iliyofungwa kistadi na Stephen Mwasika kwenye dakika ya 51 iliyompeleka Kaseja upande mwingine baada ya Davies Mwape kuangushwa ndani ya 18 na Mgosi aliisawazishia Simba kunako dakika 74 ya mchezo kwa mpira wa kichwa baada ya kipa Berko kuutema mpira wa faulo iliyopigwa na Okwi alieingia kipindi cha pili,Simba walitawala mchezo lakini Yanga walikua wakicheza Counter Attack zilizokua zikileta kizaa zaa golini mwa Simba
Mashabishi wa Yanga walipojitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao
Mashabiki wa Simba nao walikua nyomi kuipa sapoti timu yao(picha zote kwa hisani ya FULL SHANGWE)

No comments: