ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 22, 2011

RAHA YA KULEA ‘MAPACHA’ SITA

MWANAMKE yeyote aliyezaa ni dhahiri atasema kazi ya kumlea mtoto mmoja kwa kumlisha na kumweka safi ni mpambano unaoendelea kwa miaka kadhaa. Lakini, hebu fikiria kazi aliyonayo mwanamke Jenny Masche ambaye muda si mrefu uliopita alijifungua watoto sita kwa mpigo!


Kila siku Jenny (pichani kushoto), mumewe na watoto wake sita hutakiwa atayarishe chupa 38 za maziwa, awabadili nguo mara 18, afue malundo mawili ya nguo na nepi 50.

Jenny (32), ambaye ni mkazi wa Lake Hayasu, Arizona, Marekani, alizaa watoto watatu wa kiume na watatu wa kike. Licha ya matatizo aliyoyapata wakati wa kujifungua, yeye na wanaye wako katika afya njema.

Watoto hao, Bailey, Molli na Savannah (wanawake), na Blake, Cole na Grant (wanaume) wanaaminika kuwa ni ‘kundi’ la tisa duniani la watoto sita waliozaliwa pamoja na ambao wote wapo hai.

“Nilipogundua kwamba nilikuwa na watoto sita tumboni, niliogopa nikidhani huenda ningewapoteza wote, sikuamini kama ningeweza kuwabeba wote tumboni bila matatizo,” anasema Jenny.

Nchini Marekani, miaka 24 imepita tangu watoto sita kuzaliwa mara moja huko Merseyside, ambapo wote walikuwa ni wasichana na bado wanaishi.

CHANZO:GLOBAL PUBLISHERS

No comments: