Tuesday, March 15, 2011

Tangazo la Misa Kwa Kiswahili



Ndugu Watanzania na Wote wapenzi wa Lugha ya Kiswahili. Ni tumaini kubwa kuwa tuko katika kufunga na kusali. Ni Kwaresma au Mfungo Mtakatifu.
 
Kwa mara nyingine tunawakaribisha kushiriki Misa Takatifu kwa Kiswahili lugha ya Taifa letu na ya Kimataifa pia.
 
Lini?        March 20, 2011 saa 8:30 Mchana
Wapi?      St. Camillus Parish
                1600 St. Camillus Drive
                Silver Spring, MD 20903
Nani?       Mtanzania yeyote. Yeyote anayezungumza kiswahili. Na yeyote mwenye Mapenzi mema.
Nia:-  Kujiombea sisi tulioko ughaibuni na Familia zetu, Kuliombea taifa letu amani na Kumshukuru Mungu kwa Baraka tulizojaliwa. Tutamwombea kwa namna ya Pekee Padri Wolfugang Pisa OFM ambaye amechaguliwa kuwa mkuu wa Shirika lake Jimbo la Tanzania.
Kumekuwa na Ombi la Kubariki Chumvi na Maji kwa matumizi majumbani mwetu kwa kutakasa na kulinda afya. Baraka hiyo itatolewa.
Karibu - Karibuni sana.
 
Wenu Padri Evod Shao na Kamati ya Maandalizi

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake